Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UN alaani vikali shambulio la roketi Kabul

Picha ya Maktaba ikionesha sehemu ya mji wa Kabul, Afghanstan
UNAMA/Freshta Dunia
Picha ya Maktaba ikionesha sehemu ya mji wa Kabul, Afghanstan

Mkuu wa UN alaani vikali shambulio la roketi Kabul

Amani na Usalama

Mji mkuu wa Afghanistan, Kabul leo umeshambuliwa kwa roketi na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia wengi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio hilo na kutoa wito wa kumaliza mara moja machafuko nchini humo.

“Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani shambulio la leo mjini Kabul ambalo limesababisha vifo na majeruhi kwa raia . Ametuma pia salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi”imesema taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa Katibu Mkuu.

Katibu Mkuu amezungumzia pia kuhusu haja ya kukomeshwa kwa machafuko nchini Afghanistan na ameelezea matumaini kwamba mchakato wa majadiliano ya amani utapunguza machafuko hayo haraka na kukomesha mashambulizi.

“Mkutano ujao wa ASfghanistan 2020 ambao utafanyika kuanzia Novemba 23-24 ukiwaleta pamoja wawakilishi kutoka Afghanistan, Finland na Umoja wa Mataifa ni fursa ya kusisitiza ahadi ya maenedeleo ya amani na mafanikio kwa mustakabali wa taifa hilo” amesema Katibu Mkuu katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa duru za Habari zaidi ya makombora 20 yamelipuka kwenye mji mkuu Kabul leo Novemba 21 kutokana na mashambulio ya roketi ikiwemo katika eneo la  karibu na ukanda wa kijani ambako kuna majengo ya balozi mbalimbali na ifisi za kimataifa.