Watoto zaidi ya 6,500 walazimika kukimbia kila siku Syria:UNICEF
Shiriika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa wito wa kusitisha mapigani mara moja ili kuwalinda watoto na kuruhusu uingizaji wa misaada ya kibinadamu bila vikwazo.
Shiriika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa wito wa kusitisha mapigani mara moja ili kuwalinda watoto na kuruhusu uingizaji wa misaada ya kibinadamu bila vikwazo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mastaifa Antonio Guterres amesema anatiwa wasiwasi mkubwa na machafuko yanayoendelea Kaskazini Mgharibi mwa syria na ametoa wito wa kusitisha uhasama mara moja.
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock amezuru moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Jordan ya Za’atari kujionea hali halisi na kuzungumza na wakimbizi kutoka Syria.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kutokomeza Ukimwi, UNAIDS linatoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa haki ya afya kwa wote inazingatiwa kwa kupatia kipaumbele uwekezaji wa umma katika sekta ya afya.
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amelaaani vikali kuendelea kwa mauji na ufurushwaji wa raia kaskazini magharibi mwa Syria licha ya kutangazwa kwa usitijashi mapigano takriban wiki moja iliyopita.
Wakati mapigano yakiendela na watu wakiendelea kufurushwa Kaskazini magharibi mwa Syria, mahitaji ya watoto na familia kwa ujumla yanaongezeka kila uchao kwa mujibu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ijumaa limepitisha azimio la kuongeza muda wa msaada wa kibinadamu mpakani na operesheni za kibinadamu Syria, lakini kwa kupitia mpaka na Uturuki tu.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kibinadamu, OCHA imeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota jimbo la Idlib Kaskazini magharibi mwa Syria ambako zaidi ya raia milioni tatu wamezuia na vita wengi wakiwa ni wanawake na watoto
Wakati mwaka mpya ukianza na vita nchini Syria vikikaribia mwaka wa 10, hali kwa watoto wengi hususan walioko Kaskazini Magharibi mwa nchi ni mbaya sana