Watoto milioni 19 duniani walikuwa wakimbizi ndani ya nchi zao 2019- UNICEF
Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF inakadiria kuwa watoto milioni 19 duniani kote walikuwa wakimbizi wa ndani mwaka 2019, ambapo kati yao hao milioni 12 ni wakimbizi wapya kwa mwaka huo wa 2019.