Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nina wasiwasi mkubwa na machafuko yanayoendelea Syria:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.

Nina wasiwasi mkubwa na machafuko yanayoendelea Syria:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mastaifa Antonio Guterres amesema anatiwa wasiwasi mkubwa na machafuko yanayoendelea Kaskazini Mgharibi mwa syria na ametoa wito wa kusitisha uhasama mara moja.

Katika taarifa iliyotolewa leo na msemji wake Katibu Mkuu amerejea kusistiza kwamba mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu ya raia ikiwemo vituo vya huduma za afya na elimu hayakubaliki asilani.

Ametaka operesheni zote za kijeshi toka pande zote ikiwemo hatua zinazochukuliwa na makundi ya kigaidi, lazima ziheshimu wajibu na sheria za kimataifa wa sheria za kibinadamu ambazo zinajumuisha kuwalinda raia na miundombinu yao.

Katibu Mkuu ameendelea kusisitiza kwamba “hakuna suluhu ya kijeshi kwa mzozo wa Syria. Njia pekee kuelekea utulivu wa taifa hilo ni suluhu ya kisiasa inayojumuisha pande zote na kusimamiwa na umoja wa Mataifa kwa kuzingatia azimio la Baraza la Usalama nambari 2254 la mwaka 2015.”