Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msimu wa baridi waleta madhila zaidi kwa waliokimbia mapigano Idlib, Syria-UNICEF

Familia ambazo zinakaa kambini karibu na mpaka na Uturukikufuatia uhasama unaoshuhusiwa jimbo la Idlib na Aleppo.(Juni 2019)
© UNICEF/UN0318979/Ashawi
Familia ambazo zinakaa kambini karibu na mpaka na Uturukikufuatia uhasama unaoshuhusiwa jimbo la Idlib na Aleppo.(Juni 2019)

Msimu wa baridi waleta madhila zaidi kwa waliokimbia mapigano Idlib, Syria-UNICEF

Msaada wa Kibinadamu

Wakati mapigano yakiendela na watu wakiendelea kufurushwa Kaskazini magharibi mwa Syria, mahitaji ya watoto na familia kwa ujumla yanaongezeka kila uchao  kwa mujibu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

Kupitia video ya Shirika hilo la UNICEF, wanaonekana watoto, wanawake na wanaume wakitembea huku mvua zikinyesha. Makazi yao ni vyandarua tu ambapo shirika hilo linasema wakati baridi inazidi kuwa kali, familia zilizofurushwa zinakabiliwa na hali mbaya ya baridi katika mazingira ambayo ni magumu kwa watoto.

Wakimbizi hao wanaonekana wakikarabati makazi yao ili kuweza kustahimilia mvua kubwa zinazoshuhudiwa.

Tangu Desemba mwaka 2019 ongezeko la ukatili unaoshuhudiwa vijiji vya kusini mwa Idlib umewalazimu takriban watu laki tatu kukimbia makwao Maarrat An-Numan na miji mingine katika eneo hilo huku asilimia 80 ikikadiriwa kuwa ni wanawake na watoto.

Familia zilizofurushwa zimesaka hifadhi katika maeneo salama ya kusini mwa Idlib hususan mashulei na misikitini au katika makazi ya muda karibu na mpaka wa Uturuki.

Msimu wa baridi unaongeza mahitaji zaidi kwani wakazi ikiwemo vitu kama blanketi na mavazi ya kukabiliana na hali ya baridi.

UNICEF inarejelea kusisitiza kwamba ulinzi wa watoto na miundombinu ya raia ambayo wanategemea huko kasakazini magharibi mwa Syria na kote nchini ni lazima ilindwe na pande zote katika mzozo.