Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu alaani mauaji na ufurushaji wa raia Idlib, Syria

Familia inayokimbia mapigano Idlib iliweka makazi ya muida katika kambi kijiji cha Aqrabat karibu na mpaka na Uturuki. (Juni 3 2019)
© UNICEF/Aaref Watad
Familia inayokimbia mapigano Idlib iliweka makazi ya muida katika kambi kijiji cha Aqrabat karibu na mpaka na Uturuki. (Juni 3 2019)

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu alaani mauaji na ufurushaji wa raia Idlib, Syria

Haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amelaaani vikali kuendelea kwa mauji na ufurushwaji wa raia kaskazini magharibi mwa Syria licha ya kutangazwa kwa usitijashi mapigano takriban wiki moja iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR, Jeremy Laurence amewaambia waandishi wa habari kwamba Kamishna Mkuu ametoa wito kusitishwa mara moja uhasama ndani na karibu ya eneo la Idlib na kulindwa kwa raia na miundo msingi yao.

Bwana Laurence amesema, “wasiwasi mkubwa ni kuhusu usalama wa raia ambao wanaendelea kuwa hatarini, na kwamba wakati harakati za usitishwaji wa mapigano zinahitaji kufuatilliwa, makubaliano ya mwisho kabisa kama yalivyo mengine ya mwaka jana, kwa mara nyingine hayajalinda raia.

Msemaji huyo amenukuu Bachelet akisema, “inasikitisha sana kwamba raia wanauwawa kila siku katika mashambulizi ya mabomu ya anga na ardhini. Wanawake, wanaume na watoto wakiendesha shughuli zao za kila siku kazini, sokoni na shuleni wanauwawa na kujeruhiwa na ukatili usio elezeka.”

OHCHR imesema tangu kuanza kwa ongezeko la uhasama katika maeneo ya kulikositishwa mapigano Idlib na vitongoji vyake mnamo Aprili 29 mwaka 2019 hadi Januari 15 mwaka huu, timu yake imethibitisha matukio 1,506 ikiwemo wanawake 293 na watoto 433 waliuwawa. Kati ya hao raia 75 ikiwemo wanawake 17 na watoto 22 yalikuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na vikosi vya serikali.

Bwana Laurence amesema, “mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao na ukatili na kulazimika kupita maeneo ya mapigano. Wengine wamekimbilia maeneo nje ya Idlib huku wengine wakivuka na kuelekea kaskazini mwa Aleppo ambako kunashikiliwa na makundi yaliyojihami yanayoungwa mkono na Uturuki ambako kiwango vha ukatili kinasalia kuwa cha juu.”

 

TAGS: Idlib, Syria, Michelle Bachelet, OHCHR