Wengine bado wakihaha kusubiri kufungua shule, UN yatoa mwongozo wa hatua za kufuata
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa mwongozo wenye mapendekezo ya mikakati ya kiafya ya kuzingatiwa na serikali kuhusu linin a jinsi ya kufungua tena shule kwenye maeneo ambako shule bado zimefungwa kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.