Kuna faida gani Baraza la Usalama kupitisha maazimio ilhali hayaheshimiwi? - Wahoji wananchi Syria
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo wamepatiwa maswali ambayo raia, wahudumu wa kibinadamu, wawakilishi wa nchi wanachama na wahudumu wa afya wanahoji juu ya kile kinachoendelea nchini Syria, ikiwa ni miaka nane makombora na maroketi yakiendelea kumiminika kwa raia.