Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mtu ana haki ya kuishi bila woga wa wapi anapokanyaga:Guterres

Rebecca Morris anajisikia salama baada ya uteguaji wa mabomu uliofanywa na UNMAS
UNMAS
Rebecca Morris anajisikia salama baada ya uteguaji wa mabomu uliofanywa na UNMAS

Kila mtu ana haki ya kuishi bila woga wa wapi anapokanyaga:Guterres

Amani na Usalama

Watu wote wana haki ya kuishi kwa usalama na bila hofu ya wapi watakakopita au kukanyaga wakitembea.

Mabomu yakiandaliwa kwa ajili ya kuharibiwa
UNMAS
Mabomu yakiandaliwa kwa ajili ya kuharibiwa

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katiuka ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya uelimishaji na msaada wa hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini ambayo kila mwaka huadhimisha Aprili 4.

Guterres amesema katika kuelekea kutimiza ajenda ya maendeleo endelevu SDGs ya mwaka 2030 ni lazima kuondoa mabomu yote yaliyotegwa ardhini, vilipuzi ambavyo ni mabaki ya silaha za vita na vifaa vya mlipuko.

Ameongeza kuwa “hatua dhidi ya mabomu hayo zinasafisha njia na kuweka mazingira salama ambayo nyumba zinaweza kujengwa , pia hatua hiyo inabadili fikra za watu ili kujua jinsi gani wanaweza kujilinda na zinawapa wat una jamii fursa na matumaini mapya.”

Katibu Mkuu amesema kwa miaka 20 Umoja wa Mataifa umekuwa ukizisaidia nchi kuwa huru dhidi ya vitisho na hatari ya mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vingine vya mlipuko na mwaka huu Umoja wa Mataifa umezindua kampeni mpya “viwanja salama” ili kuhakikisha kwamba “hakuna mtu , hakuna taifa na hakuna uwanja wa vita unaoachwa nyuma” Guterres amesema kwa kampeni hii ya kimataifa lengo ni kuhakikisha tunabadilisha viwanja vilivyosheheni mambomu ya ardhini kuwa viwanja vya michezo na kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika na manusura wa vita.

Walinda amani wa UN kutoka CHad wakikagua mabomu ya kutegwa ardhini yanayotumiwa na vikundi vya kigaidi huko Mali.
UN /Sylvain Liechti
Walinda amani wa UN kutoka CHad wakikagua mabomu ya kutegwa ardhini yanayotumiwa na vikundi vya kigaidi huko Mali.

Naye balozi mwema wa ofishi ya Umoja wa Mataifa inayohusiska na uelimishaji na uteguaji wa mabomu ya ardhini na vifaa vingine vya mlipuko UNMAS mcheza filamu nyoja Daniel Craig amesema hatua za kujivunia zimepigwa katika vita hivi japo amechagiza juhudi zaidi akisema, “hadi sasa nchi 164 zimeridhia au kusaini mkataba kuhusu mabomu hayo, nchi 88 zimeetegua na kuharibu mabomu milioni 50 yaliyotengwa ardhini. Nchi 31 zilizokuwa na mabonu yaliyotegwa ardhini sasa yameteguliwa, haya ni mafanikio makubwa yanayostahili kusherehekewa . Yamefanikishwa na uelimishaji, kuchukizwa nayo, kwa juhudi za wanaharakati, hadi kazi za mashirika ya asasi za kiraia “

Hata hivyo amesema mafanikio haya yasizifanye nchi kubweteka na kwamba hatua zaidi zinahitajika ili kuyatokomeza kabisa.