Kuchangia CERF ni uwekezaji bora zaidi- Guterres
Kuwekeza katika mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF si tu kunafanikisha usaidizi wa kibinadamu bali pia ni kuwekeza katika kuboresha kazi za chombo hicho chenye wanachama 193, amesema Katibu Mkuu Antonio Guterres jijini New York, Marekani hii leo wakati akifungua kikao cha ngazi ya juu cha kuchangia mfuko huo ulioanzishwa mwaka 2006.