Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yatoa ombi kubwa zaidi kuwahi kutolewa kuwafikia watoto wengi walio na mahitaji

Watoto walioyakimbia mapigano mjini Idlib Syria
©UNICEF/Watad
Watoto walioyakimbia mapigano mjini Idlib Syria

UNICEF yatoa ombi kubwa zaidi kuwahi kutolewa kuwafikia watoto wengi walio na mahitaji

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa ombi lake la dharura la dola bilioni 4.2 kuwasaidia watoto milioni 59 na msaada wa kuokoa katika nchi 64 kote duniani. Ndilo ombi kubwa zaidi likiwa mara tatu zaidi ya lile lilotolewa mwaka 2010.

Mmoja kati ya watoto wanne anaishi katika nchi zinazoathiriwa na mizozo na majanga kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore. Anasema watoto wengi zaidi wanalazimika kuhama makwao wakiwa kwa dharura wanahitaji ulinzi na misaada.

Idara inayoshughulikia huduma za kibinadamu kwa watoto ya UNICEF ina malengo ya kuwapa watoto waliaothiriwa na mizozo na majanga na maji, huduma za usafi, lishe, elimu, afya na huduma za usalama. Wakijumuishwa watu wazima, ombi hilo litatoa huduma za dharura kwa watu milioni 95.

Maombi matano makubwa zaidi ni kwa wakimbizi nchini Syria na jamii zinazowapa makao nchini Misri, Jordan, Lebanon, Iran na Uturuki kwa dola milioni 864.1, Yemen dola mlioni 535, Syria dola milioni 294.8, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo dola milioni 262.7 na Sudan Kusini dola milioni 180.5.

Uwezo wetu wa kuwasaidia watoto kuanzia wakati janga linapotokea hadi wakati watarejea maisha yao kawaida inahitaji ufadhili unaopatikana kwa haraka na ambao si wa kutumiwa kwa nchi fulani au suala fulani. Ufadhili ambao unatusadia kuokoa maisha zaidi, alisema Fore.

Mwaka 2019 ufadhili unaopatikana kwa haraka uliiwezesha UNICEF kuchukua hatua za haraka katika masuala ya usalama na watu wanaohama makwao nchini Burkina Faso na Mali nchi mbili ambazo maombi yao yalipata ufadhili mdogo.