Watu 70 wameshapata chanjo ya Ebola DRC na chanjo 11,000 kuwasili Guinea Jumapili:WHO
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linaongeza juhudi zake za kukabiliana na mlipuko mpya wa ebola nchini Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linaongeza juhudi zake za kukabiliana na mlipuko mpya wa ebola nchini Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisema ukosefu wa uwiano katika mgao na utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona, au COVID-19 ni tishio kubwa katika kutokomeza ugonjwa huo ambao hadi sasa umesababisha vifo vya watu milioni mbili duniani kote.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limeanza kutoa chanjo dhidi ya Ebola kwa wakazi wa eneo la Butembo jimboni Kivu Kaskazini, ikiwa ni wiki moja baada ya mgonjwa mmoja kuthibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.
Makundi yaliyojihami huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, yameendelea kutekeleza mauaji na vitendo vya kikatili na dhalili kwa wakazi wa enoe hilo hata mwaka huu wa 2021.
Kikosi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT_7 kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kimetamatisha jukumu lake rasmi na kukabidhi bendera kwa kikosi cha 8 au TANZBATT_8. Shuhuda wetu kutoka Beni, jimboni Kivu Kaskazini ni Luteni Issa Mwakalambo, afisa habari wa TANZBATT_7.
Kikosi cha 8 cha Tanzania, TANZBATT-8 kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO.
Kufuatia serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutangaza kifo cha mtu mmoja huko Butembo jimboni Kivu Kaskazini kutokana na ugonjwa wa Ebola, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limepeleka wafanyakazi zaidi na linajiandaa kupeleka vifaa vya matibabu.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, inasikitishwa na ongezeko kubwa la matukio ya mashambulizi ya raia kwenye maenoe ya Irumu na Mambasa jimboni Ituri halikadhalika eneo la Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Noela Kombe al maaruf Mamaa Noela ni mwanamke shujaa aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kujitolea kulea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu licha ya kuwa na changamoto nyingi anazo kumbana nazo wakati wa uendeshaji wa kituo hicho cha Mungu ni Mwema kilichopo eneo la Beni mjini jimboni Kivu kaskazini nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
Hatimaye matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Umoja wa Mataifa kwa wakazi wa dunia kuhusu udharura wa janga la tabianchi yametolewa hii leo huku asilimia 64 ya washiriki wakitambua umuhimu wa hatua za dharura dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na hivyo kuwepo kwa hatua mahsusi za makusudi ili kukabili janga la tabianchi linalokumba dunia hivi sasa.