Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo dhidi ya Ebola zaanza kutolewa Butembo, DRC 

Jinsi chanjo ya ebola inavyopatiwa binadamu ili kumkinga na ugonjwa huo. Pichani ni wakati wa mlipuko huko Equateur ambapo Dkt. Alhassane Toure anampatia chanjo mhudumu wa afya katika kituo cha Mbandaka, nchini DRC
WHO/Lindsay Mackenzie
Jinsi chanjo ya ebola inavyopatiwa binadamu ili kumkinga na ugonjwa huo. Pichani ni wakati wa mlipuko huko Equateur ambapo Dkt. Alhassane Toure anampatia chanjo mhudumu wa afya katika kituo cha Mbandaka, nchini DRC

Chanjo dhidi ya Ebola zaanza kutolewa Butembo, DRC 

Afya

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limeanza kutoa chanjo dhidi ya Ebola kwa wakazi wa eneo la Butembo jimboni Kivu Kaskazini, ikiwa ni wiki moja baada ya mgonjwa mmoja kuthibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Eneo la Butembo ni eneo ambalo lilikuwa kitovu cha mlikuwa wa 10 uliotangazwa kumalizika mwezi Juni mwaka jana. 

Utoaji huo wa chanjo kwa kuangazia zaidi wale walio hatarini kupata maambukizi ya Ebola, umeanzia ukanda wa kiafya wa Biena katika hospitali ya Matanda mjini Butembo, ambako mgonjwa wa kwanza alipatiwa matibabu kabla ya kufariki dunia kutoka na Ebola

Utoaji chanjo pia unafanyika katika ukanda wa afya wa Katwa mjini Butembo. 

Hadis as watu wanne wamethibitishwa kuwa na Ebola na watu wawili wamefariki dunia. 

Takribani dozi 1200 za chanjo ziliwasilisha Butembo wiki iliyopita na dozi nyingine 1200 zimewasili Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini. 

WHO ina uhakika kuwa DRC ina dozi za kutosha za chanjo dhidi ya Ebola kwa ajili ya kuchanja watu 16,000. 

Kwa mujibu wa WHO, chanjo zilizopo zinatosha kuchanja wahudumu wa afya na watu wengine walio hatarini zaidi kupata maambukizi. 

Wiki iliyopita, serikali ya DRC ilitoa taarifa ya kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola jimboni Kivu Kaskazini.