Watu 70 wameshapata chanjo ya Ebola DRC na chanjo 11,000 kuwasili Guinea Jumapili:WHO 

Mlipuko wa ebola umeripotiwa nchini Guinea. (Maktaba)
WHO/Junior D. Kannah
Mlipuko wa ebola umeripotiwa nchini Guinea. (Maktaba)

Watu 70 wameshapata chanjo ya Ebola DRC na chanjo 11,000 kuwasili Guinea Jumapili:WHO 

Afya

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linaongeza juhudi zake za kukabiliana na mlipuko mpya wa ebola nchini Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. 

Akizungumza leo kwenye mkutano na waandioshi wa Habari mjini Brazzaville Jamhuri ya Congo, mkurugenzi wa Who kanda ya Afrika Dkt. MoMatshidiso Moet amesema juhudi hizo ni pamoja na kuimarisha ufuatuliaji wa wagonjwa, watu waliokutana nao, upimaji, matibabu pamoja na maandalizi ya chanjo. 

“Tunajitahidi san ana tunakwenda mbio kudhibiti virusi hivyo. Tukiwa na wataalam na vifaa tayari mashinani , ni mwanzo mzuri”. 

Nchini Gunea Ndege ya misaada ya kibvinadamu imewasili Nzerekore juma hili ikiwa na shehena za zaidi ya kilo 700 za vifaa tiba vilivyotolewa na Who na washirika wake. 

Na zaidi ya dozi 11,000 za chanjo dhidi ya Ebola zinatarajiwa kuwasili nchini humo  Jumapili ya tarehe 21  Februari wiki hii. 

Uandaaji wa chanjo ya ebola katika maabara hospitali ya Donka, Conakry, Guinea
WHO/S. Hawkey
Uandaaji wa chanjo ya ebola katika maabara hospitali ya Donka, Conakry, Guinea

Dozi 20,000 zimepangwa kutolewa Guinea 

Dkt. Moeti amesema mbali ya dozi 11,000 zitakazowasili Jumapili hii Guinea , kuna dozi zingine 8, 500 zitashafirishwa kutoka Marekani hadi nchini humo na kufanya jumla ya dozi kuwa takriban 20,000. 

Kwa mantiki hiyo WHO imesema chanjo itaanza hivi karibuni na kuongeza kuwa timu ya wataamu 30 wa kutoa chanjo wameashaandaliwa. 

Nchini humo wahudumu wa WHO wako tayari kupelekwa maeneo ya vijijini ya Guniea punde chanjo itakapowasili.  

Pia shirika hilo linapeleka wataalam kuisaidia wizara ya afya ya Guniea na inatarajiwa kushiriki katika kuongeza kasi ya hatua za kudhibiti ugonjwa huo ili usisambae zaidi. 

Wahudumu hao zaidi ya 100 wa WHO waliopelekwa Guinea nan chi zingine wanatarajiwa kushiriki vita hivyo dhidi ya ebola ifikapo mwisho wa mwezi Februari. 

Timu nyingine ya wataalam 8 wa kutoka ofisi ya WHO Africa inatarajiwa kuondoka hivi karibuni kuelekea Guinea. 

Kwa ujumla WHO na washirika wake wanashirikiana kwa karibu na timu ya kitaifa kujenga uwezo katika maeneo yote muhimu ya ufuatiliaji nah atua za kukabiliana na mlipuko huo. 

Dkt. Moeti “Juhudi zetu na hatua zetu za pamoja ni muhimu katika kuepuka kusambaa zaidi kwa ebola hasa wakati huu ambao badi janga la corona au COVID-19 linaleta changamoto na limeshatoa shinikizo kubwa kwa wahudumu wa afya na vituo vya afya.” 

Muhimu kubaini visa mpakani 

Kwa sababu kitovu cha mlipuko wa Ebola nchini Guinea ni maeneo ya mpakani nchini za mpakani ziko katika tahadhari kubwa. 

Nchi hizo jirani zinaimarisha hatua za afya ya umma na ufuatiliaji katika miji na jamii za mpakani. 

Lengo ni kubaini haraka na kuchukua hatua haraka uwezekano wa wagonjwa mpakani. Hatua zinazoendelea hivi sasa nchini Guinea na maandalizi na maandalizi nchi jirani zinatokana na uzoefu uliopatika wakati wa mlipuko wa awali wa Ebola Afrika Magharibi  kati ya mwaka 2014-2016. 

Hadi kufikia sasa katika mlipuko huu mpya nchini Guinea watu 7 wanaaminika kuambukizwa virusi vya Ebbola katika eneo la Kusini Mashariki mwa nchi hiyo na miongoni mwao 5 wameshafariki dunia. 

Congo DRC hali ilivyo 

Kwa upande wake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imeripoti wagonjwa wanne waliothibitishwa kuwa na Ebola ikiwemo vifo viwili. 

Mashariki mwa nchi hiyo WHO ina takriban wataalam 20 ambao wanazisaidia mamlaka za afya za taifa na kikanda. 

Takriban dozi 8,000 za chanjo bado zilikuwepo nchini humo wakati ulipomalizika mlipuko wa 11 wa Ebola. 

Chanjo kwa watu ambao wako katika hatari kubwa zaidi ilizinduliwa rasmi Februari 15 Butembo Mashariki mwa DRC ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa. 

Zaidi ya watu 70 wameshapatiwa chanjo Butembo 

Hadi kufikia leo karibu watu 70 wameshapatiwa chanjo DRC. Kupelekwa haraka kwa chanjo ni ushuhuda tosha uwezo uliojengwa katika eneo hilo na WHO na wadau wengine katika mlipuko uliopita. 

WHO imetoa dola milioni 1.25 kusaidia hatua za kukabiliana na ugonjwa huo nchini Guinea  na kuimarisha maandalizi katika nchi jirani za Cote d’Ivoire, Guinea-Bissai, Liberia, Mali, Senegal na Sierra Leone. 

Zaidi ya hapo mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetoa dola milioni 15 kusaidia juhudi za kupambana na mlipuko huo nchini Guinea na DRC.