Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Mandhari ya milima mjini Sharm El-Sheikh, na Qesm Sharm Ash Sheikh, Misri
Unsplash/Juanma Clemente-Alloza

COP27: Unachohitaji kufahamu kuhusu mkutano mkubwa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa la mwaka huu.

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu unafanyika huko Sharm el-Sheikh,nchini Misri wakati ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.

Hussein Juma Hassan mnufaika wa mradi wa ILO wa kutambua na kurasimisha mafunzo ya awali anasema anapenda zaidi kazi ya kuchomelea vyuma katika malori na matrekta.
© ILO/OIT Belinda Japhet

Simulizi ya Hussein Juma Hassan: Kufeli masomo si kufeli maishani

Nilipopata fursa ya kusoma ili nipate cheti cha kutambuliwa rasmi kuwa mchomeleaji vyuma mwenye stadi, sikuchelea bali nilikuwa na hamu ya kuchukua fursa hiyo. Awali sikuwa na uthibitisho wa stadi hiyo na uzoefu niliokuwa nao ulitokana na kufanya kazi hii kwa miaka 25 na kujifunza nikiwa kazini. Ni simulizi ya Hussein Juma Hassan kutoka Zanzibar, Tanzania, baba wa familia ya mke na watoto 6.

Ales Bialiatski wa pili kushoto wakati wa hafla ya tuzo ya Wlodkowic kenye bunge la Poland mwaka 2014
© Michał Józefaciuk

Washindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2022 watangazwa 

Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel ya Norway leo imetangaza washini wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2022 kuwa ni "Mtetezi wa haki za binadamu Ales Bialiatski kutoka Belarus, shirika la haki za binadamu la Urusi Memorial na shirika la haki za binadamu la Ukraine Center for Civil Liberties ambao wanawakilisha jumuiya za kiraia katika nchi zao.” 

Wanafunzi wakishiriki katika mpango wa elimu katika kituo cha Kashonjwa nchini Uganda
© UNICEF/ Zahara Abdul

Elimu sio ufunguo wa maisha tu ni msingi wa maendeleo:UN 

Elimu ni nguzo muhimu katika jamii na ndio ufunguo wa maisha. Ili kuleta usawa katika jamii, juhudi nyingi zimeongezwa kasi ili bidhaa hiyo iwafikie watoto na vijana wa jinsia zote mbili kwa mujibu wa ripoti ya karibuni iliyotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa japo imetoa angalizo kwamba maeneo ya vijijini bado yamesalia nyuma hata baada ya harakati kuimarishwa.