Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Washindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2022 watangazwa 

Ales Bialiatski wa pili kushoto wakati wa hafla ya tuzo ya Wlodkowic kenye bunge la Poland mwaka 2014
© Michał Józefaciuk
Ales Bialiatski wa pili kushoto wakati wa hafla ya tuzo ya Wlodkowic kenye bunge la Poland mwaka 2014

Washindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2022 watangazwa 

Haki za binadamu

Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel ya Norway leo imetangaza washini wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2022 kuwa ni "Mtetezi wa haki za binadamu Ales Bialiatski kutoka Belarus, shirika la haki za binadamu la Urusi Memorial na shirika la haki za binadamu la Ukraine Center for Civil Liberties ambao wanawakilisha jumuiya za kiraia katika nchi zao.” 

Kamati imeoneza kuwa kwa miaka mingi watetezi hao “wamekuza haki ya kukosoa mamlaka na kulinda haki za msingi za raia. Wamefanya juhudi kubwa kuorodhesha uhalifu wa kivita, ukiukwaji wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka. Kwa pamoja wanaonyesha umuhimu wa jumuiya ya kiraia kwa amani na demokrasia.” 

Kuhusu Ales Bialiatski 

Ales Bialiatski alikuwa mmoja wa waanzilishi  wa vuguvugu la demokrasia lililoibuka Belarus katikati mwa miaka ya 1980.  

Amejitolea maisha yake kuchagiza maendeleo ya demokrasia na amani katika nchi yake. 

Miongoni mwa mambo mengine alianzisha shirika la Viasna (Spring) mwaka 1996 kufuatia marekebishop ya katiba yaliyoleta utata ambayo yalimpa rais mamlaka ya kidikteta na kusababisha maamndamano makubwa. 

Shirika la Viasna lilikuwa likitoa msaada kwa waandamanaji waliofungwa jela na familia zao. 

Na katika miaka iliyofuata shirika hilo likageuka kuwa shirika la haki za binadamu likiorodhesha na kupinga matumizia ya nguviu na utesaji uliofanywa na mamlaka dhidi ya wafungwa wa kisiasa. 

Serikali imejaribu mara kadhaa kumnyamazisha Ales Bialiatski. Alifungwa jela mwaka 2011 hadi 2014 ikifuatia maandamano makubwa ya kupinga serikali.. 

Na mwaka 2020 alikamatwa ten ana mpaka sasa  bado anashikiliwa bila kesi kusikilizwa. 

Licha ya changamoto zote hizo Bwana Bialiatski hajakata tamaa ya kupigania haki za binadamu na demokrasia Belarus.  

Shirika la haki za binadamu la Memorial 

 Shirika la haki za binadamu la Memorial lilianzishwa mwaka 1987 na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu katika muungano wa zamani wa Soviet ambao walitaka kuhakikisha kwamba  waathirika wa utawala wa ukandamizaji wa Kikomunisti hawatosahaulika. 

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Andrei Sakharov na mtetezi wa haki za binadamu Svetlana Gannushkina walikuwa miongoni mwa waanzilishi. Ukumbusho unatokana na dhana kwamba kukabili uhalifu wa zamani ni muhimu katika kuzuia uhalifu mpya. 

Baada ya kuanguka kwa muungano wa Sovieti, ukumbusho uligeuka na kuwa shirika kubwa zaidi la haki za binadamu nchini Urusi.  

Mbali na kuanzisha kituo cha haki za wahasiriwa wa enzi ya Stalinist, kituo hicho kiuikusanya na kuratibu habari juu ya ukandamizaji wa kisiasa na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Urusi.  

Shirika hilo likawa chanzo chenye mamlaka zaidi cha habari juu ya wafungwa wa kisiasa katika vituo vya kizuizini vya Urusi. 

Kituo cha Uhuru wa Kiraia  

Kituo cha Uhuru wa Kiraia kilianzishwa huko Kyiv mwaka 2007 kwa madhumuni ya kuendeleza haki za binadamu na demokrasia nchini Ukraine.  

Kituo hicho kimechukua msimamo wa kuimarisha jumuiya ya kiraia ya Ukraine na kushinikiza mamlaka kuifanya Ukraine kuwa nchi yenye demokrasia kamili.  

Ili kuiendeleza Ukrainie kuwa taifa linalotawaliwa na sheria, Kituo cha Uhuru wa Kiraia kimetetea kwa dhati kwamba Ukrainie ihusishwe na mahakama ya kimataifa ya uhalifu. 

Baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine Februari 2022, Kituo cha Uhuru wa Kiraia kimejishughulisha na juhudi za kutambua na kuweka kumbukumbu za uhalifu wa kivita wa Urusi dhidi ya raia wa Ukraine.  

Kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa, kituo hiki kinatekeleza jukumu la mtari wa mbele  kwa nia ya kuwawajibisha wahusika kwa uhalifu wao. 

Baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 2022, Kituo cha Uhuru wa Kiraia kimejishughulisha na juhudi za kutambua na kuweka kumbukumbu za uhalifu wa kivita wa Urusi dhidi ya raia wa Ukraine. Kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa, kituo hiki kinatekeleza jukumu la upainia kwa nia ya kuwawajibisha wahusika kwa uhalifu wao. 

  Kwa kutoa tuzo ya amani ya Nobel ya 2022 kwa Ales Bialiatski, shirika la Memorial na Kituo cha Uhuru wa Kiraia, kamati ya Nobel ya Norway inapenda kuwaenzi mabingwa hawa watatu bora wa haki za binadamu, demokrasia na kuishi pamoja kwa amani katika nchi jirani za Belarus, Urusi na Ukraine.  

Kupitia juhudi zao za kuunga mkono maadili ya kibinadamu, kupinga uvamizi wa kijeshi na kanuni za sheria, washindi wa mwaka huu wamefufua na kuheshimu maono ya Alfred Nobel ya amani na udugu kati ya mataifa, maono yanayohitajika zaidi duniani kote hii leo.