UNWTO yatangaza orodha ya vijiji 32 Bora vya Utalii duniani
Kutoka Austria hadi Vietnam, maeneo 32 kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni yametajwa kuwa 'Vijiji Bora vya Utalii kwa mwaka 2022' na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO).
Kutoka Austria hadi Vietnam, maeneo 32 kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni yametajwa kuwa 'Vijiji Bora vya Utalii kwa mwaka 2022' na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO).
Watu milioni 100 wamelazimishwa kuondoka makwao mwaka wa 2022 na Umoja wa Mataifa uliendelea kusaidia wale wanaohitaji msaada kwa njia nyingi, na kuchagiza njia zaidi za kisheria, na salama za watu kuhama.
Wakati huu ambapo hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyesajiliwa katika mji mkuu wa Uganda tangu tarehe 14 Novemba, 2022 mamlaka ya afya ya Mji Mkuu wa Kampala kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya nchi hiyo hivi karibuni ilifanya kampeni ya siku saba kuelimisha umma ili kudumisha umakini wa watu na hatimaye kusaidia kumaliza mlipuko wa ugonjwa huo hatari duniani.
Kama ilivyo kwa vijana wengi wa Côte d'Ivoire, makuzi ya Hervé kwa kiasi kikubwa yamepata ushawishi kutoka kwenye vyombo vya habari. “Vilitufanya tuamini kuwa maisha ni bora zaidi barani Ulaya,” anasema Hervé.
Mkutano wa 15 au COP 15 wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu bayoanuai, CBD unaendelea mjini Montreal Canada ukizikutanisha serikali kutoka kote duniani na wadau wengine muhimu kwa lengo la kuafikiana malengo mapya yatakayoiongoza dunia katika hatua za kubadili mwelekeo na kusitisha upotevu wa bayoanuai ambayo ni tegemeo la viumbe na mazingira ifikapo mwaka 2030.
Siku 16 za uhamasishaji jamii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake zikiendelea kote duniani leo tunakupeleka Sudan, kutana na Semira anaeishi kwenye kambi ya Otash nchini huko ambaye ameonja shubiri ya ukatili wa kijinsia.