Watoto 33,000 hatarini kufa nchini Ethiopia- UNICEF
Takriban watoto 33,000 katika eneo ambalo halifikiki la Tigray nchini Ethiopia wana utapiamlo mkali na wanakabiliwa na vifo iwapo msaada wa haraka hautapatikana, imesema taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Henrietta Fore iliyotolewa leo jijini New York, Marekani.