Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Kuta katika eneo la Shualah kwenye mji mkuu wa Iraq, Baghdad ukiwa na picha za kuelimisha familia jinsi ya kupatia matibabu mgonjwa wa COVID-19 pindi wanapokuwa nyumbani

IRAQ yashauriwa kutoa kipaumbele kwa makundi hatarishi

UNAMA
Kuta katika eneo la Shualah kwenye mji mkuu wa Iraq, Baghdad ukiwa na picha za kuelimisha familia jinsi ya kupatia matibabu mgonjwa wa COVID-19 pindi wanapokuwa nyumbani

IRAQ yashauriwa kutoa kipaumbele kwa makundi hatarishi

Ukuaji wa Kiuchumi

Ripoti mpya mbili zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zimesema lazima kipaumbele kitolewe katika mikakati ya kujikwamua na janga la corona au COVID-19 kwa makundi yaliyo hatarini nchini Iraq wakiwemo wanawake, vijana na wakimbizi wa ndani ili kuhakikisha ujumuishwaji na uendelevu katika kujikwamua huko.

Ripoti hizo zilizotolewa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani UNDP, shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-HABITAT na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM zimetokana na utafiti ulioangalia athari za coronavirus">COVID-19 katika masuala ya kiuchumi na kijamii na maisha katika ngazi ya kaya, ukijikita zaidi kwenye makundi yaliyo hatarini kama wanawake, vijana, watoto, watu wenye ulemavu na jamii zilizotawanywa. 

Pia ripoti imelinganisha mazingira ya mijini na vijijini na kuangalia athari katika ngazi ya serikali ya shirikisho la Iraq na jimbo la Kurdistan.

UNDP imekuwa ikifuatilia athari za janga la Corona na kutoa ripoti nchini Iraq kila mara ambapo mpaka sasa jumla ya ripoti 7 zimeshatolewa.

"COVID-19 imeleta na itaendelea kuleta madhara ya muda mrefu kwa makundi hatarishi nchini Iraq katika kujitafutia riziki, usalama wa chakula, afya na elimu hususan kwa wanawake, vijana, wazee, walemavu na wakimbizi wa ndani" amesema mwakilishi mkaazi wa UNDP nchini Iraq Zena Ali Ahmad.

Zena ameshauri serikali ya Iraq, mji wa Kurdistan pamoja na wadau ndani ya nchi hiyo kusaidia harakati za kuwainua wananchi walioathirika na janga la corona.

"Kama ripoti ilivyoonesha Zahiri shahiri, bila kutilia mkazo kundi hili hatarishi , Iraq inaweza shindwa kufikia malengo yake ya muda mrefu na kuhatarisha harakati za kufikia malengo yaliyojiwekea ifikapo mwaka 2030"