Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Ndege ya abiria ya Ryanair ikiwa uwanja wa ndege nchini Italia. ( Picha maktaba)

Mambo 5 unayopaswa kufahamu kuhusu ICAO: Shirika la Umoja wa Mataifa la Anga

Unsplash/Lucas Davies
Ndege ya abiria ya Ryanair ikiwa uwanja wa ndege nchini Italia. ( Picha maktaba)

Mambo 5 unayopaswa kufahamu kuhusu ICAO: Shirika la Umoja wa Mataifa la Anga

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Katika kujibu kile kinachoelezwa kuwa tukio la ndege ya kibiashara kulazimishwa kutua katika Mji Mkuu wa Belarus, Minsk, Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Anga, ICAO, liliitisha mkutano wa dharura wa kidiplomasia siku ya Alhamisi. Je ICAO inasema nini kuhusu tukio hilo, na ina nguvu gani?

1) ICAO ilisababisha kuzaliwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la anga

Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia kilikuwa ni kipindi cha maendeleo makubwa kwenye upande wa teknolojia ya masuala ya anga.  Mwishoni mwa vita vya pili vya dunia, mwaka 1944 katika kile kilichohisiwa uwezekano wa kuwa na idadi kubwa ya watu na safari za ndege, serikali ya Marekani iliwakaribisha mataifa washirika wake kwenda mjini Chicago kuzungumzia uundwaji wa mkataba wa kwanza wa Kimataifa kuhusu Usafiri wa Anga, ujulikanao kama “Mkataba wa Chicago”  
Lengo kuu la shirika hili ni kuhakikisha kunakuwa na maendeleo ya anga ya kimataifa “katika hali ya usalama na utulivu” na kuanzisha huduma za usafiri wa anga “katika misingi ya usawa wa fursa na uendeshaji mzuri na wakiuchumi.”
Mwaka 1947, Shirika la Umoja wa Mataifa la anga - ICAO likaanzishwa rasmi , lenye jukumu la kuratibu na kusaidia ushirikiano wa wa kimataifa ambao ungehitaji kuwa na mtandao mpya wa usafirishaji wa anga. 
Makao makuu ya ICAO yapo mjini Montreal, Canada.  
 

Wawakilishi walikutana mjini Chicago nchini Marekani mwaka 1944, ambao waliandika mswada wa kuanzisha mkataba wa kimataifa wa usalama wa anga.
ICAO
Wawakilishi walikutana mjini Chicago nchini Marekani mwaka 1944, ambao waliandika mswada wa kuanzisha mkataba wa kimataifa wa usalama wa anga.

2) Shirika linahakikisha kuna utendaji mzuri wa shughuli za anga ulimwenguni

Kwa mujibu wa Mtandao wa usafiri wa unga, Shirika hili ni mmoja ya mifano mizuri na hai wa mahusiano wa kimataifa unaohakikisha mtandao unafanya kazi kwa ufanisi, kuhakikisha kila mtu anafuata sheria walizojiwekea. Hili linasalia kuwa jukumu muhimu zaidi la ICAO. 
 Lina jishughulisha katika kufanya tafiti kuhusu sera mpya za usafiri, kuleta uwiano kwenye ubunifu, linafanya hafla kuangalia maendeleo mapya katika sekta ya anga na pia kutoa ushauri kwa serikali jinsi ya kuanzisha viwango vipya vya kutoa mapendekezo ambayo yameonesha yanafanya kazi kwenye sekta ya anga.
Pia wanatoa elimu, kukuza ushirikiano, kufanya ukaguzi, mafunzo na kufanya shughuli nyingine za kujengea uwezo ulimwenguni.


3) … Haifanyi kazi kama polisi wa anga

Kama ilivyo kwa umoja wa Mataifa kwa ujumla, nguvu ya ICAO ipo kwenye kuleta pamoja nchi wanachama kwa idadi kubwa, kuunda mikataba ya kimataifa. Hata hivyo sio mdhibiti, na halina uwezo wa kusimamia usalama angani.
ICAO haiwezi kuifungia au kuizuia anga ya nchi, kufunga njia za anga, au kulaani viwanja vya ndege au mashirika ya ndege kwa utendaji mbovu, au huduma duni kwa wateja. Nchi zina jukumu la kujiwekea kanuni zake, waendeshaji wa shughuli za ndege ni lazima wazifuate pindi waingiapo kwenye anga la nchi hiyo na wawapo katika viwanja vya ndege. 
Kama nchi itavunja makubaliano ambayo yamekubaliwa kimataifa na kupitishwa na ICAO, jukumu la wakala litakuwa ni kusaidia nchi kupata majibu yaliyotarajiwa. 
 

Ndege ya Raynair ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege
Unsplash/Fotis Christopoulos
Ndege ya Raynair ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege

 4) ICAO  ina wasiwasi mkubwa na tukio lililotokea Belarus

Jumapili ya tarehe 23 Mei 2021, ndege ya shirika la Ryanair ikitokea Ugiriki kwenda Lithuania iliripotiwa kubadilishwa masafa na kwenda uwanja wa ndege wa Minsk, nchini Belarus ambapo abiria kadhaa waliamriwa kushuka ndani ya ndege akiwemo mwandishi wa habari maarufu, Roman Protasevich.  
Nchi kadhaa zimelaani tukio hilo, mashirika ya haki za binadamu pamoja na Umoja wa Mataifa: Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres alionesha wasiwasi wake mkubwa na kutaka kuwepo kwa uchunguzi kamil na uchunguzi wa haki na Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Shirika la Umoja wa Mataifa -OHCHR amesema namna Mwandishi huyo (Protasevich) alivyotekwa nyara na kuletwa Belarus “ilikuwa sawa na tafsiri isiyo ya kawaida.”   
ICAO ilizungumzia suala hilo kupitia mtandao wake wa Twitter siku ya tukio hilo, walikiri “kuwa na wasiwasi mkubwa kwa kitendo cha kulazimishwa kutua kwa ndege ya Ryanair na abiria wake, ambacho kinaweza kuwa ni kinyume cha mkataba wa Chicago.” Siku moja baadae ICAO ikatangaza tena kupitia Twitter kuitisha mkutano wa dharura tarehe 27 Mei 2021. 


 5) ……. Nini inaweza kufanya?

Hili sio tukio la kwanza kutokea kwa ndege kubadilishwa muelekeo na kutua kwa lazima, lakini baadhi ya wataalamu wanaamini hii ni mara ya kwanza ICAO inakuwa na mazungumzo kwa kuwa mwanachama wake anashutumiwa kuhusika katika tukio hilo.
Hata hivyo Belarus kwa upande wake imeendelea kushikilia msimamo wake kuwa kuamuru ndege hiyo kushuka ilikuwa ni lazima kwa sababu kulikuwa na tishio la bomu, na imepinga vikali kuwa tukio hilo lilikuwa ni la kupagwa kichochezi.
Inawezekana mkutano ulioitishwa na ICAO “ukasababisha kuwepo kwa uchunguzi huru” kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alivyohimiza, lakini kama ilivyo elezwa hapo awali , Wakala huu sio mdhibiti wa anga na haina nguvu ya kuchukua maamuzi yeyote dhidi ya Belarus, kama vile kufunga anga ya nchi hiyo wala kuwawekea vikwazo.
Wakati huo huo Muungano wa nchi za Ulaya -EU umetangaza kuiwekea Belarus vikwazo vya kiuchumi na kutangaza kuzuia ndege za Belarus kuingia katika anga ya Muungano wa Ulaya na viwanja vya ndege. 
Uamuzi huo umekaribishwa na Marekani ambapo utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani umesema unatathmini “maamuzi yanayofaa.”