Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Cali, jiji lililoko magharibi mwa Colombia.

COLOMBIA: UN yalaani mauaji ya waandamanaji mjini Cali

UN News/Laura Quinones
Cali, jiji lililoko magharibi mwa Colombia.

COLOMBIA: UN yalaani mauaji ya waandamanaji mjini Cali

Haki za binadamu

Natoa wito wa kukomeshwa kwa aina yeyote ya vurugu, pamoja na uharibifu, na pande zote kuendeleza mazungumzo, na kuhakikisha maisha ya watu na utu unaheshimiwa na watu wote" Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amepaza sauti kulaani vikali tukio la hivi karibuni nchini Colombia katika mji wa Cali, ambapo ripoti zinaonesha tangu tarehe 28 Mei, watu 14 wamekufa , watu 98 wamejeruhiwa, na 54 kati yao na watu wenye silaha wakati vurugu zilipoibuka katika mji huo ambapo maandamano yalikuwa yanafanyika kuadhimisha mwezi mmoja wa maandamano makubwa ya kitaifa.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na ofisi yake mjini Geneva, Uswisi, Bi.Bachelet amesema amepokea tarifa ya watu wenye silaha, pamoja na askari wa mahakama wasiokuwa kazini, kuwamiminia risasi waandamanaji, waandishi wa habari waliokuwa wakiripoti maandamano hayo, pamoja na waenda kwa miguu.

Afisa huyo wa mahakama aliyetajwa alipigwa na waandamanaji mpaka kufa. Na kwa mujibu wa taarifa katika maeneo mengine ya mji, watu binafsi wamepiga risasi kuwaelekezea waandamanaji mbele ya polisi.

"Matukio haya yanatia wasiwasi, ikizingatiwa maendeleo yaliyofikiwa katika kutafuta suluhu kupitia majadiliano, machafuko yaliyozuka mwezi uliopita, kufuatia kuanza kwa mgomo wa kitaifa kupinga sera kadhaa za kijamii na kiuchumi za serikali." Amesema Bachelet

Ameongeza kuwa "Ni muhimu wale wote walioripotiwa kusababisha watu kujeruhiwa na kuuwawa, ikiwemo watendaji wa serikali, uchunguzi kuanza haraka wa huru na haki, bila upendeleo, kwa uwazi na kwamba watakao patikana na hatia kuchukuliwa hatua" 

"Natoa wito wa kukomeshwa kwa aina yeyote ya vurugu, pamoja na uharibifu, na pande zote kuendeleza mazungumzo, na kuhakikisha maisha ya watu na utu unaheshimiwa na watu wote" amesema kamishna Bachelet akisisitiza mazungumzo ndio yatapatia suluhu mahitaji ya makundi yote, wale wanaoandamana na wale wanaopinga maandamano.

Amewapongeza wale wote waliopaza sauti mjini Cali na ngazi ya kitaifa kutafuta suluhu na kwa amani kupitia mazungumzo.

Ofisi ya haki za binadmu ya Umoja wa Mataifa nchini Colombia pia imepokea taarifa ya kukamatwa kwa takriban watu 30 tarehe 28 Mei.

"wale waliokamatwa na kuwekwa kizuizini wafanyiwe mahojiano na uchunguzi kwa haki" amesema Bachelet kufuatia kuzuka kwa wasiwasi wa walipo wale waliokamatwa na kuwekwa kizuizini akisisitiza mambo yote yafanyike kwa kuzingatia viwango vya haki za binadamu vya kimataifa.