Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Ndege zisizo na rubani zinaweza kuleta huduma karibu na watu naishio vijijini

Ndege isiyo na rubani kupunguza vifo wakati wa kujifungua nchini Botswana

© UNFPA Botswana
Ndege zisizo na rubani zinaweza kuleta huduma karibu na watu naishio vijijini

Ndege isiyo na rubani kupunguza vifo wakati wa kujifungua nchini Botswana

Afya

Ndege zisizo na rubani zinaokoa Maisha ya wanawake waishio vijijini nchini Botswana, ambao huenda wangepoteza maisha, shukran kwa Umoja wa Mataifa.

Kwa wanawake wa Botswana, hususan wanaoishi katika maeneo ya vijijini ambako kuna uhaba wa dawa na hakuna damu ya akiba, kujifungua kunaweza kuwa jambo la kuhatarisha maisha.

Takwimu za mwaka 2019 za vifo vitokanavyo na kujifungua, zilionesha uwiano wa vifo 166 kwa kila wakina mama 100,000 wanaojifungua, idadi hii ni mara mbili ya idadi ya watu wenye uwezo wa kati na wajuu kiuchumi katika nchi hiyo.

Mwezi huu wa Mei, Shirila la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA, Serikali ya Botswana Pamoja na chuo kikuu cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia nchini Botswana (BIUST) waliungana kuzindua mradi maalum wa "ndege isiyo na rubani kwa afya".

Beatrice Mutali, Muwakilishi Maazi wa UNFPA nchini Botswana anaamini mradi huu utabadili kabisa hali iliyopo sasa, nakwamba si tu utaboresha huduma ya kujifungua nchini humo, bali utabadili taswira nchima ya utoaji huduma ya afya nchi nzima.

"Katika UNFPA, tuna maono ya Dunia ambayo hakuna mwanamke anakufa wakati wa kujifungua, na mpango kama huu unalenga kufuta vifo vya kina mama wakati wa kujifungua nchini Botswana".

Muuguzi akiweka mzigo wa dawa za matibabu kwenye ndege isiyo na rubani kabla haijaanza safari.
© UNFPA Botswana
Muuguzi akiweka mzigo wa dawa za matibabu kwenye ndege isiyo na rubani kabla haijaanza safari.

 

Mutali ametolea mfano kituo cha afya cha Mogapi, kilichopo kijijini ambako kina hudumia zaidi ya watu 3,000 ambacho kitanufaika na huduma ya haraka itakayotolewa na ndege hizo zisizo na rubani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, waziri wa afya nchini Botswana, Dkt. Edwin Gorataone Dikoloti amesema "hitaji la kuwekeza kwenye ubunifu ambao utasaidia kuziba pengo la umbali mrefu, utapunguza gharama za usafirishaji, utaepuka changamoto za miundombinu, na kuboresha upatikanaji wa dawa za dharura, bidhaa na huduma muhimu za dharura kwa hiyo ni la haraka."

Naye Lorato Mokganya, afisa mkuu wa afya, Wizara ya afya ya Botswana ameeleza kuwa "mwanamke akipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua na ikiwa anatakiwa kupelekwa hospitali ya rufaa, kwanza atatakiwa kuwekwa sana kabla hajahamishwa kutoka katika zahanati. Kuhakikisha damu inapatikana kwa wakati inaweza kuoka maisha. Ndege zisizo na rubani ziaweza kutumwa kupeleka damu ili mgonjwa awekewe"

Katika juhudi za kuzuia vifo vinavyoweza kuzuilika na kupatia ufumbuzi changamoto za kijiografia, mpango huu wa kufikisha huduma kwanjia ya ubunifu umeleta mapinduzi katika kusambazaji wa vifaa vya matibabu na nchini Botswana

 

Kwa mujibu wa Dkt Dimane Mpoeleng, msimamizi wa mradi huo na mhadhiri wa sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu cha BIUST, kila ndege ina betri yenye uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa 100 na ina uwezo wa kubeba mzito wenye uzito wa kilo 2.

Vijiji 4 vya majaribio vimechaguliwa katika kutekeleza mradi huu

"kutoa huduma kwa wakati kwa wajawazito ambao wamepata changamoto wakati wa kujifungua ni jambo la msingi, hususan katika maeneo ya pembezoni na magumu kufikika." Amesema Mpoeleng,

 

Kufikiwa lengo namba 3 la SDG

Chanzo kikuu cha vifo wakati wa kujifungua nchini Botswana, ni kutokwa na damu nyingi, changamoto baada ya mimba kutoka na shinikizo la damu wakati wa ujauzito.

Kupitia mradi huu, Botswana inakuwa nchi ya kwanza kwa upande wa kusini mwa Afrika na nchi ya tatu kwa bara la Afrika baada ya Ghana na Rwanda kuwa na mradi huu ambapo ndege isiyo na rubani inatumika kutoa msaada wa afya.

wanajamii wakitazama ndege isiyo na rubani iliyotua katika kituo cha afya cha Moremi
© UNFPA Botswana
wanajamii wakitazama ndege isiyo na rubani iliyotua katika kituo cha afya cha Moremi

 

Mwaka 2017, Botswana ilijiwekea malengo ya kupunguza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua ikidhamiria vifo 71 kwa kila Watoto 100,000 wanaojifungua ifikapo mwaka 2025, na kupungua zaidi mpaka 54 ifikapo mwaka 2030 ili kufikia lengo namba 3 la maendeleo endelevu la milenia - SDG.

Iwapo hali iliyopo sasa haitabadilika basi Botswana inaweza ikashindwa kufikia lengo hilo ililojiwekea.

Mradi huu unategemewa kuleta mabadiliko makubwa na kupunguza muda wa kusafirisha mahitaji kutoka saa kadhaa mpaka dakika kadhaa, kusaidia huduma za kujifungua na kuoka maisha ya watu wengi zaidi.