Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Nchini Niger, mashambulio dhidi ya raia na vikundi visivyo vya serikali na operesheni za kijeshi zimekuwa zikiongezeka, na kufungwa kwa mipaka na hatua zingine za kuzuia COVID-19 zimesababisha maalum yaliyoko hatarini kuathirika.
© UNICEF/Juan Haro

Nchi 1 kati ya 8 ndio zenye mipango ya kulinda wanawake dhidi ya athari za COVID-19: UN 

Takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women na lile la mpango wa maendeleo UNDP kuhusu hatua za kimataifa za kukabiliana na janga la corona au COVID-19 katika suala la kijinsia zinaonyesha kwamba mikakati ya hifadhi ya jamii na masuala ya ajira wakati wa janga hili imeyapa kisogo mahitaji ya wanawake. 

© UNICEF/Frank Dejongh

Afrika, hatua tulizochukua dhidi ya COVID-19 zimedhihirishia ulimwengu uthabiti wetu.

Fikra za baadhi ya watu kuwa maelfu kwa maelfu ya watu barani Afrika watapukutika kutokana na janga la ugonjwa wa Corona, au COVID-19 zimekuwa ndivyo sivyo baada ya bara hilo kuchukua hatua kitaifa na kikanda na hatimaye hadi sasa kudhihirisha umuhimu wa mshikamano katika kukabili adui. Hilo limebainishwa wakati wa hotuba za marais waliohutubia mjadala mkuu wa mkutaon wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao kutokana na vikwazo vilivyopo Marekani kutokana na janga la Corona.

Sauti
6'4"
Mwanafunzi wa kike nchini Ghana akinawa mikono kwa sabuni kabla ya kurejea darasani ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali kuhakikisha elimu inaendelea huku wakidhibiti maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
UNICEF/Geoffrey Buta

Hatua tulizochukua dhidi ya COVID-19 zimedhihirishia ulimwengu uthabiti wetu Afrika 

Fikra za baadhi ya watu kuwa maelfu kwa maelfu ya watu barani Afrika watapukutika kutokana na janga la ugonjwa wa Corona, au COVID-19 zimekuwa ndivyo sivyo baada ya bara hilo kuchukua hatua kitaifa na kikanda na hatimaye hadi sasa kudhihirisha umuhimu wa mshikamano katika kukabili adui. Hilo limebainishwa wakati wa hotuba za marais waliohutubia mjadala mkuu wa mkutaon wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao kutokana na vikwazo vilivyopo Marekani kutokana na janga la Corona. Flora Nducha anamleta Assumpta Massoi ambaye amefuatilia hotuba za viongozi hao na anaeleza kwa kina.

Sauti
6'4"
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA75 kwa njia ya video.
UN Photo/Evan Schneider

Hakuna nchi hata moja inaweza peke yake kumudu janga kama hili la COVID-19

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hii leo akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa njia ya vdeo iliyorekodiwa kutokana na janga la virusi vya corona kutoruhusiu viongozi wa dunia kukutana New York Marekani kama ilivyo ada ya kila mwaka, ameueleza ulimwengu kuwa ugonjwa wa COVID-19 linapaswa kutoa msukumo mpya, “kwa juhudi zetu za pamoja za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.” Na hakuna nchi ambayo peke yake inaweza kumudu janga kubwa la kiwango cha COVID-19.