Nchi 1 kati ya 8 ndio zenye mipango ya kulinda wanawake dhidi ya athari za COVID-19: UN 

28 Septemba 2020

Takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women na lile la mpango wa maendeleo UNDP kuhusu hatua za kimataifa za kukabiliana na janga la corona au COVID-19 katika suala la kijinsia zinaonyesha kwamba mikakati ya hifadhi ya jamii na masuala ya ajira wakati wa janga hili imeyapa kisogo mahitaji ya wanawake. 

Kwa mujibu wa takwimu hizo ni nchi 1 tu kati ya 8 kote duniani ndizo zilizo na mipango ya kuwalinda wanawake dhidi ya athari za kiuchumi na kijamii zilizoletwa na janga la COVID-19.  

Takwimu hizo za ripoti ya pamoja ya ufuatiliaji “COVID-19 ufuatiliaji wa hatua za kupambana na janga hilo za mlengo wa kijinsia (1)” ambayo imejumuia Zaidi yah atua 2,500 kwenye nchi 206 imetathimini hususan hatua za serikali kwa jicho la kijinsia kwenye mambo matatu ambayo ni “wale wanaokambiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana(VAWG), msaada kwa huduma zisizo na malipo na kuimarisha usalama wa kiuchumi kwa wanawake.” 

Matokeo yaliyopatikana 

Kwa mujibu wa UN Women na UNDP matokeo ya tathimini hiyo yameonyesha kwamba nchi 42 ikiwa ni asilimia 20 ya waliofanyiwa tathimini, hazina kabisa hatua maalum zenye mlengo wa jinsia katika kukabiliana na COVID-19. 

Nchi 25 pekee ambazo ni saw ana asilimia 12 ya dunia ndizo zilizoanzisha hatua ambazo zinazingitaa maeneo matatu muhimu yaliyotajwa na ripoti hii nah atua hizo zinaweza kujumuisha utoaji msaada, malazi au hatua za kisheria kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wakati wa janga la COVID-19, kugawa fedha taslimu kunakoelekezwa kwa wanawake, utoaji wa huduma za kulea watoto au klipa familia na likizo ya ugonjwa. 

Akizungumzia takiwmu hizo mkurugenzi mtendani wa UN Women Phumzile Mlanbo-Ngcuka amesema “Ni bayana kwamba janga la COVID-19 linawagonga vibaya wanawake , kama waathirika wa ukatili majumbani hatua za kusalia majumbani zimewalazimisha kusalia na wakatili wao, pia kama watoa huduma pasi kulipwa katika familia na jamii na kama wafanyakazi katika kazi ambazo hazina ulinzi wa hifadhi ya jamii. Mkakati wa kimataifa wa ufuatiliaji unazisaidia serikali kufanya maamuzi bora ya kisera kwa kushirikiana nao mifano bora na mchakato wa ufuatiliaji katika sera za huduma nah atua za kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake.” 

Naye mkuu wa UNDP Achim Steiner kwa upande wake amesema “Mgogoro wa COVID-19 unatoa fursa kwa nchi kufanyia mabadiliko muundo uliopo wa kiuchumi na kuingia katika mikakati mipay ya kijamii ambayo inatoa kipaumbele kwa haki ya kijamii na usawa wa kijinsia. Mkakati huu mpya wa ufuatiliaji wa masuala ya kijinsia unaweza kusaidia kuchapuza mabadiliko ya kisera kwa kuzingatia mapengo katika juhudi za kitaifa na ufadhili na kutanabaisha mifano bora.” 

Mambo ambayo serikali nyingi zimejikita nayo 

Takwimu hizo mpya zinaonyesha kwamba serikali zimejikita zaidi katika jududi zinazohusiana na jinsia kupambana na COVID-19 hasa katika kuzuia au kuchukua hatua kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, nah atua hizo ni asilimia 71 ya hatua zote zilizobainishwa au sawa na mikakati 704 katika nchi 135. 

Na kati ya hizo asilimia 63 wamejikita katika kuimarisha huduma muhimu kama malazi, mfumo wa kuomba msaada na michakato mingine ya utoaji taarifa.  

Hata hivyo asilimia 48 tu ya nchi ambazo ni chini yar obo ya nchi zote zilizofanyiwa tahimini zimezichukulia huduma za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana (VAWG) kama sehemu ya miakati yah atua zao za kitaifa na kijamii ya kupambana na COVID-19 huku zikiwa na fungu dogo san ana fedha za kuziefadhili. 

Wakati huohuo takwimu zimeonyesha kwamba huduma za hifadhi ya jamii, za migogoro na changamoto za ajira zimefumbia macho mahitaji ya wanawake kukiwa na mikakati 177 pekee ambayo ni sawa na asilimia 10 katika nchi 85 ambayo ndio inalenga kuimarisha ulinzi wa kiuchumi kwa wanawake na chini ya theluthi moja ya nchi zote (nchi 60) ndio zinazochukua hatua kusaidia huduma zisizo na malipo na kuimarisha huduma za malezi ya watoto, wazee au watu wenye ulemavu. 

Tofauti baina ya nchi 

Tathimini hiyo pia imeonyesha kwamba hatua zinazochukuliwa kuhusiana na masuala ya usawa wa kijinsia zinatofautiana baina ya nchi na kanda. 

Ulaya imeelezwa kuongoza katika hatua za kushughulikia VAWG na huduma zinazotolewa pasi ujira ambavyo ni takriban asilimia 32 ya hatua zote za kupambana na ukatili na asilimia 49 na hatua zote za kushughulikia huduma zote zinazotolewa pasi ujira. 

Bara la Amerika ndilo lenye idadi kubwa na hatua zenye kulenga kuimarisha ulinzi kwa kiuchumi kwa wanawake likifutiwa na bara la Afrika. 

 Mwisho kabisa tathimini hiyo imesisitiza kwamba hata katika nchi ambazo zimeweka hatua mbalimbali za mrengo wa kijinsia , hatua hizo zitakuwa na maana endapo kutakuwa na ufadhili wa kutosha  na zikiwa endelevu. 

 

TAGS: UNDP, UN Women, VAWG, usawa wa kijinsia, COVID-19, coronavirus

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter