Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemi Alade: Niko tayari kujitolea kwa nguvu zangu zote kufanikisha malengo ya UNDP

Yemi Alade: Niko tayari kujitolea kwa nguvu zangu zote kufanikisha malengo ya UNDP

Pakua

Mwanamuziki Yemi Alade, raia wa Nigeria ambaye hivi karibuni ametangazwa kuwa Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP amesema malengo ya UNDP yanaendana na malengo yake kwa hivyo atajitolea kwa uwezo wake wote.  Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Mkuu wa shirika hilo, Achim Steiner akimkaribisha Yemi, amesema Balozi huyo anajiunga na familia ya Umoja wa Mataifa katika kipindi ambacho COVID-19 imeuvuruga ulimwengu lakini wana matumaini naye. Steiner anasema, "kufikia mwaka 2021, ikiwa ni matokeo ya janga la COVID-19, kunaweza kuwa na wanawake 180 wanaoishi katika ufukara kati ya wanaume 100. Asilimia 68 ya wanyama pori wametoweka ulimwenguni tangu mwaka 1970 na kila mwaka dunia inapoteza misitu ambayo kwa ukubwa ni zaidi ya nchi ya Denmark. Kwa kuunganisha sauti yake yenye nguvu na UNDP, ninafahamu kuwa Yemi atainua uongozi wa wanawake na vijana katika kusaidia kubadili mwenendo huu mbaya. Karibu katika familia ya Umoja wa Mataifa. Karibu UNDP. Asante Yemi.” 

Naye Yemi Alade akizungumza kupitia video, ameahidi kuweka juhudi zake zote kutimiza malengo ya UNDP akisema, “ni heshima kutajwa kuwa Balozi mwema wa UNDP. Shirika ambalo mipango yake inaendana na yangu kabisa kabisa. Niko tayari kufanya kazi nao kwa pamoja ili kuhakikisha ahueni kwa wote na hivyo ndivyo tunaweza kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu kufikia mwaka 2030. Na Niko tayari kutoa sauti yangu kwa makusudio ya UNDP” 

 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'46"
Photo Credit
UN Photo/Paulo Filgueiras