Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UNICEF/Josue Mulala

DRC Shule zikifunguliwa, dawati moja mwanafunzi 1 ili kuepusha COVID-19

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imeitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kufungua shule ili wanafunzi wanaofanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi na sekondari waweze kuendelea masomo yao licha ya kuwepo kwa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo taifa hilo la maziwa makuu. Ahimidiwe Olotu na taarifa zaidi.

Sauti
1'55"
Ushirika wa mataifa ya Kusini-SSC- umetoa mafunzo ya maelekezo kuhusu ulimaji wa mpunga Cote D'ivoire.
©FAO/Wang Jinbiao

Ushirikiano baina ya nchi za kusini umekuwa jawabu wakati huu wa COVID-19

Utashi wa ushirikiano baina ya nchi za kusini au zile zinazoendelea na mshikamano wa dunia bado uko hai ulimwenguni kote wakati huu ambapo tunahaha kukabiliana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya ushirikiano wa nchi za kusini hii leo.
 

OHCHR Regional Office for Centra

Catalina:Tunataka watambue kuwa kuna binadamu wanaojali binadamu wenzao

Catalina, si jina lake halisi, ni mwanasheria kutoka Nicaragua mwenye umri wa miaka 44 na ambaye alikimbilia nchi jirani ya Costa Rica ili kunusuru maisha yake na ya watoto wake wawili. Flora Nducha na maelezo zaidi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema kuwa Catalina hivi sasa ni mkimbizi Costa Rica. 

Mwaka 2018 wakati wa maandamano dhidi ya serikali nchini Nicaragua, Catalina alifungua milango ya nyumba yake ili kusaidia waandamanaji ambapo aliwapatia chakula pamoja na huduma ya kwanza pindi walipopata majeruhi. 

Sauti
2'21"
© UNHCR/Rocco Nuri

Watoto wakimbizi wahusishwa katika kupambana na COVID-19 Uganda

Mlipuko wa COVID-19 duniani umetia mashakani karibu malengo yote ya Maendeleo endelevu au SDGs baada ya kukwamisha elimu, usafiri na uchumi miongoni mwa mengine. Hali imekuwa mbaya zaidi miongoni mwa wakimbizi kutokana na changamoto za uhaba wa rasilimali ambazo kawaida huwakumba hasa idadi yao inapoongezeka  bila kutarajiwa. Hata hivyo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake nchini Uganda wameanzisha ushirikishwaji wa watoto wakimbizi katika juhudi za kupambana na COVID-19 wakati huu ambapo takribani wakimbizi mia moja wameambukizwa. Je, wanashirikishwa vip

Sauti
3'24"
Utafiti wa kutafuta Chanjo ya virusi vya Corona unaendelea
Unsplash

Mtandao wa maabara mahsusi za kunyumbua virusi vya Corona yazinduliwa Afrika

Wakati nchi za Afrika zikiendelea kupanua huduma za upimaji wa virusi vinavyosababisha Corona au COVID-19, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na kituo cha Afrika cha udhibiti na kinga ya magonjwa, Africa CDC, wamezindua mtandao wa maabara ili kuimarisha hatua za kuchambua na kufuatilia mnyumbuliko wa virusi vya Corona aina ya 2 kinachosababisha shida kwenye mfumo wa hewa, SARS-CoV-2.
 

© UNICEF/UNI312809// Frank Dejongh

Ripoti yaonesha COVID-19 yaweza futa mafanikio ya kupunguza vifo vya watoto wachanga 

Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na taasisi zake, imeonesha kuwa mafanikio yaliyopatikana takribani miongo mitatu katika kuepusha vifo vya watoto wachanga yanaweza kufutwa na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa. 

Ikiwa na makadirio mapya ya vifo vya watoto wachanga, ripoti hiyo inasema kuwa idadi ya vifo imepungua kutoka milioni 12.5 mwaka 1990 hadi vifo milioni 5.2 mwaka wa 2019. 

Sauti
2'8"