Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Kila saa mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi unaongezeka:Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi unazidi kuwa mbaya zaidi kila saa.
COVID-19 yaweza futa mafanikio ya kupunguza vifo vya watoto wachanga- Ripoti
Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na taasisi zake, imeonesha kuwa mafanikio yaliyopatikana takribani miongo mitatu katika kuepusha vifo vya watoto wachanga yanaweza kufutwa na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa.
Redio 500 za sola zatolewa na UNMISS kusaidia watoto kusoma wakati huu wa COVID-19
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umegawa redio 500 zinazotumia sola kwa jamii za Yambio , jimbo la Equatoria Magharibi ili kuwasaidia watoto waliosalia majumbani kutokana na janga la corona au COVID-19 kuweza kusoma. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.
Katika moja ya vijiji vya Yambio watoto wakiwa wamekusanyika nje pamoja wakisikiliza masomo kwa njia ya Redio ambazo zimesambazwa na UNMISS.
Shoroba za UN zitakuwa kimya,UNGA 75 itafanyika kupitia mtandao, mambo 5 ya kuyafahamu
Kikao cha 75 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 75) kitaanza rasmi Septemba 15, na mwaka huu kutokana na janga la corona au COVID-19 linaloendelea mjadala utakuwa tofauti kabisa kuwahi kutokea katika historia ya chombo hicho kinachotimiza miaka 75 mwaka huu.
UNMISS yagawa redio 500 za sola kusaidia watoto kusoma wakati huu wa COVID-19
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umegawa redio 500 zinazotumia sola kwa jamii za Yambio , jimbo la Equatoria Magharibi ili kuwasaidia watoto waliosalia majumbani kutokana na janga la corona au COVID-19 kuweza kusoma.
Licha ya changamoto waalimu, wazazi na wanafunzi wadhamiria kusoma wakati wa COVID-19 Uganda
Ugonjwa wa Corona au COVID-19 ukiendelea kusababisha baadhi ya nchi kufunga shule na vyuo na hivyo wanafunzi kulazimika kusomea majumbani, walimu, wazazi na wanafunzi nchini Uganda, wamezungumzia changamoto wanazokumbana nazo kama anavyoelezea Ahimidiwe Olotu.
Wazazi na wanafunzi washika hatamu kwenye masomo Uganda wakati huu wa Corona
Gonjwa wa Corona au COVID-19 likiendelea kusababisha baadhi ya nchi kufunga shule na vyuo na hivyo wanafunzi kulazimika kusomea majumbani, walimu, wazazi na wanafunzi nchini Uganda, wamezungumzia changamoto wanazokumbana nazo.
Mchakato wa upatikanaji na usamabazaji wa chanjo za COVID-19 kuongozwa na UNICEF
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF litafanya kazi kwa karibu na makumpuni wazalishaji wa madawa na washirika wengine katika uhakikisha upatikanaji wa dozi za chanjo ya Corona au COVID-19, usafirishaji, na uhifadhi wake kwa niaba ya kituo cha kimataifa cha COVAX. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.
UNICEF kuongoza mchakato wa upatikanaji na usamabazaji wa chanjo za COVID-19
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF litafanya kazi kwa karibu na makumpuni wazalishaji wa madawa na washirika wengine katika uhakikisha upatikanaji wa dozi za chanjo ya Corona au COVID-19, usafirishaji, na uhifadhi wake kwa niaba ya kituo cha kimataifa cha COVAX.
Uganda, UNHCR yaimarisha juhudi za kudhibiti COVID-19 miongoni mwa wakimbizi
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake nchini Uganda wameimarisha juhudi za kudhibiti vifo na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 miongoni mwa wakimbizi wakati huu ambapo wakimbizi 89 tayari wameambukizwa ugonjwa huo, huku wawili wakiripotiwa kufariki dunia. John Kibego na taarifa zaidi.