Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© Julius Mwelu/ UN-Habitat

Mapambano dhidi ya COVID-19 Kenya

Watu waliopoteza maisha hadi sasa kote duniani kutokana na virusi vya corona ikiwa imevuka 20,000 huku zaidi ya watu nusu milioni kote duniani wakiambukizwa virusi hivyo hatari nchini Kenya kama zilivyo nchi nyingine, mapambano dhidi ya ugonjwa huo yanaendelea. Katika makala ya leo, mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi anaangazia tahadhari ambazo watu wa Kenya wanazichukua kujikinga na virusi vya corona na changamoto wanazokumbana nazo.

Sauti
6'6"
UN News/ Stella Vuzo

Elimu kwa jamii kuhusu kuzuia kuenea kwa virusi vya corona Tanzania

Wakati ulimwengu unaendelea na mapambano dhidi ya virusi vya corona, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaeleza wasiwasi wake kuhusu elimu ya watoto kutokana na ulazima wa kufungwa kwas hule katika mataifa takribani 120 hivi sasa duniani kote. Shirika hilo linasema zaidi ya nusu ya wanafunzi wote ulimwenguni wameathiriwa na hatua ya kufungwa kwa shule ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutokomeza ugonjwa huo.

Sauti
4'5"
©UNICEF/Leonardo Fernandez

Katika vita dhidi ya virusi vya corona, COVID-19, kitu kikubwa tunaambiwa tuzingatie usafi: Wananchi Geita

Serikali kote duniani zimeendelea kuja na mbinu za kila namna ili kupambana na janga la virusi vya corona, COVID-19. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa nalo kwa kila namna limeendelea kuziunga mkono jitihada za nchi kote duniani ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo ya namna nzuri ya kupambana na ugonjwa huu, msingi mkubwa ukiwa kwanza utoaji elimu kwa wananchi ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi zaidi.

Sauti
3'53"