Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ramani mpya ya WFP yadhihirisha athari za COVID-19 katika mlo shuleni

Mlo shuleni kwa maelfu ya watoto ambao hawahudhuri shule umekwamishwa na uwepo wa COVID-19
WFP/Ratanak Leng
Mlo shuleni kwa maelfu ya watoto ambao hawahudhuri shule umekwamishwa na uwepo wa COVID-19

Ramani mpya ya WFP yadhihirisha athari za COVID-19 katika mlo shuleni

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limezindua ramani mpya ya kidijitali inayodhihirisha athari za virusi vya Corona, COVID-19 katika program zake za mlo mashuleni.

Kwa mujibu wa WFP ramani hiyo ambayo ni ya “ufuatiliaji wa kimataifa wa mlo mashuleni wakati wa kufungwa shule kutokana na mlipuko wa COVID-19 inatoa inatoa maenedeleo mapya ya kila siku kuhusu kufungwa kwa shule na idadi ya Watoto ambao hawapati tena mlo mashuleni kutokana na janga hili la Corona.

Mbali ya kuonyesha idadi ya jumla ya kimataifa ramani hiyo pia inaonyesha ni Watoto wangapi walioathirika katika kila nchi kwa taarifa ambazo ni za wakati huohuo na pia changamoto na haja ya kusaka suluhu.

Kwa mujibu wa takwimu mpya za WFP zaidi ya watoto wa shule milioni 364 hivi sasa wanakosa mlo shuleni ambao wamekuwa wakiutegemea.

Hatua ya kufungwa kwa shule zote au asilimia kubwa ya shule kumeripotiwa katika nchi 48 ambako WFP inaendesha program yam lo mashuleni.

Kwa mantiki hiyo WFP inaema hatua hii inamaanisha kwamba karibu Watoto milioni 11 hawapati tena mlo shuleni wa WFP na idadi hiyo inattarajiwa kuongezeka katika siki na wiki zijazo.