Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zanzibar yachukua hatua kukabili COVID-19

Zanzibar yachukua hatua kukabili COVID-19

Pakua

Katika kuepusha kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua hatua katika sekta ya mahakama ikiwemo kusitisha kwa muda usikilizaji wa kesi za madai na jinai.

Hatua hizo zimetangazwa hii leo huko Vuga, Unguja na Mrajis Mkuu wa Mahakama Mohamed Ali Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Zanzibar akisema..
(Sauti ya Mohamed Ali Mohamed)
 Na kuhusu kesi zenye dhamana na kuepusha mrundikano kwenye vyuo vya mafunzo, Bwana Mohamed amesema,
(Sauti ya Mohamed Ali Mohamed) 

Amesema ingawa Zanzibar bado haina mfumo wa kuendesha kesi kwa njia ya video, bado wanachukua hatua kuweza kuona jinsi gani wanapunguza mrundikano gerezani na rumande.
Hadi hivi sasa Zanzibar ambayo inaunda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, ina mgonjwa mmoja tu wa virusi vya Corona ilihali Tanzania Bara wamethibitishwa wagonjwa 13 hadi leo Alhamisi.

Audio Credit
UN News/ Omar Abdullah (TV washirika)
Audio Duration
2'47"
Photo Credit
UN Environment