Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

WFP/Shada Moghraby

Kambini Zaatar Jordan maandalizi dhidi ya COVID-19 yashika kasi:UNHCR

UNHCR imesema inafanya kazi na wizara ya afya ya Jordan kuandaa mazingira ya kupambana na virusi vya corona. 

Iyad Shyauiat, ambaye ni Afisa afya katika UNHCR anasema, “tunawapa mwongozo kuhusu taratibu wanazozifanya ndani ya kiliniki zao kwa maana ya kudhibiti maambukizi na kujiandaa na utayari.”

UNHCR imesema hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote wa COVID-19 ambaye ameshapatikana miongoni mwa wakimbizi ndani ya kambi lakini hospitali ndani ya kambi ambayo inawahudumia wakimbizi wa Syria takribani 76,000, inajiandaa kwa mlipuko wa ugonjwa huo.

Sauti
1'30"
UNMISS

UNMISS yashirikiana na Sudan Kusini kujiandaa kwa ajili ya COVID-19

Soko la kila wiki huko Sakure, karibu na mpaka kati ya Sudani Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC limefungwa kama sehemu ya juhudi za Serikali ya Sudani Kusini kudhibiti tishio la kimataifa la virusi vya corona au COVID-19

Soko hilo lilikuwa na shuhguli nyingi kila Ijumaa huku wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili wanakutana na kubadilishana bidhaa, lakini, serikali ya Sudani Kusini hivi karibuni imetangaza kufungwa kwa mipaka yake na nchi jirani. Na hatua hiyo imesababisha soko kufungwa pia.

Sauti
2'43"

02 APRILI 2020

Katika Jarida la habari hii leo assumpta Massoi anakuletea

-Siku ya uelimishaji kuhusu usonji ikiadhimishwa leo Umoja wa Mataifa umetoa wito kuhakikisha watu hao wanajumuisha katika harakati za kupambana na janga la virusi vya Corona , COVID-19

-Huko nchini Suda Kusini japo bado hakuna mgonjwa yeyote wa virusi vya Corona COVID-19 mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS kwa kushirikiana na serikali wachukua hatua kujikinga ikiwa ni pamoja na kufunga soko kubwa mpkani wa nchi hiyo na DRC

Audio Duration
12'59"
Mahmood ambaye ana usonji akiwa ameshika herufi P ambayo aliambiwa aitafute kwenye boksi darasani nchini Misri
© UNICEF/Rehab El-Dalil

Janga la COVID-19 linawaweka watu wenye usonji katika hatari kubwa.

Kupitia ujumbe wake maalum kwa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema siku ya uelimishaji kuhusu usonji inaadhimishwa kwa kutambua na kusherehekea haki za watu wenye usoni na kwamba “Mwaka huu siku hii inaadhimishwa katikati ya janga la kimataifa la kiafya ambalo hatujawahi kulishuhudia katika maisha yetu, janga ambalo linawaweka watu wenye usonji katika hatari kubwa kutokana na virusi vya Corona na athari zake katika jamii.”

Mpishi Ron Pickarski akikatakata mboga jikoni kwake Boulder Colorado
©FAO/Benjamin Rasmussen

COVID-19 ikitikisa, mlo uwe vipi?

Wakati wazazi wengi wanatafuta milo iliyokwishapikwa tayari na vyakula vya kusindikwa kama njia ya haraka na ya bei nafuu ya kulisha familia, kuna njia mbadala rahisi, za bei nafuu na zenye afya  hasa wakati huu wa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19

Mji wa London, Uingereza
Unsplash/Ali Yaqub

Pato la kimataifa kushuka kwa asilimia 0.9 mwaka  2020 sababu ya COVID-19:DESA

Uchumi wa dunia unaweza kushuka kwa asilimia 0.9 mwaka huu wa 2020 kutokana na janga la virusi vya Corona, COVID-19, na uzalishaji wa dunia utashuka hata zaidi endapo vikwazo vya kiuchumi vitaendelea katika robo ya tatu ya mwaka huu, na kama bajeti za kupambana na janga hili hazitosaidia kipato na wateja, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo Jumatano na Umoja wa Mataifa.

Nchi zilizoendelea kama Marekani, watoto wanaendelea na masomo kwa njia ya mtandao wakiwa nyumbani katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona
© UNICEF/Lisa Adelson

Kufungwa kwa shule kulikosababishwa na COVID-19 kutawaathiri vibaya sana wasichana-UNESCO

Kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, COVID-19 kulazimisha kufungwa kwa shule katika nchi 185 duniani, Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na shirika la Plan International limeonya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa idadi ya watoto watakaoacha shule suala ambalo litawaathiri zaidi wasichana wadogo na hivyo kuongeza pengo la jinsia katika elimu na hivyo kusababisha kuongezeka kwa hatari zaidi unynyasaji wa kingono, mimba za utotoni na ndoa za kulazimishwa na pia zile za mapema.