Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© UNICEF/Ilvy Njiokiktjien

TB ikichanganyika na COVID-19 ni janga juu ya janga

Ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB, bado umesalia kuwa miongoni mwa magonjwa hatari zaidi duniani. Zaidi ya watu 4000 hupoteza maisha yao  kila siku kutokana na ugonjwa TB huku 30,000 wakiwa wanapata maambukizi ya ugonjwa huu unaoweza kuzuiwa na kutibiwa. Gonjwa hili linasalia kuwa tishio wakati huu ambapo kumeibuka virusi vya ugonjwa wa Corona au COVID-19 ambao nao umetikisa dunia ukisambaa katika mataifa 189 na ukiwa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 14,500 tangu kubainika mwezi Desemba mwaka jana.

Sauti
4'
UN Photo - Jean-Marc Ferre

OHCHR yataka vikwazo ziondolewe kusaidia wagonjwa wa COVID-19

Wakati idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 ulimwenguni ikizidi kupaa na kuwa zaidi ya 330,000 huku vifo vikifikia 1,4652, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Michelle Bachelet ametaka vikwazo vya kisekta duniani viondolewe ili mataifa yaweza kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
 
(Taarifa ya Grace Kaneiya)
 

Sauti
2'7"
WHO

Uwepo wa COVID-19 usitufanye tusahau kuhusu tishio la TB

Tunapopambana na janga la kimataifa la afya COVID-19 ni wakati pia wa kutafakari na kutoyapa kisogo maradhi mengine makubwa ikiwemo kifua kikuu au TB, amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO. Flora Nducha na taarifa zaidi

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Mkurugenzi huyo Dkt. Tedros Adhamon Ghebreyesus ameikumbusha dunia na kila mtu kwamba ingawa virusi vya corona, COVID-19 ndio vinavyogonjwa vichwa vya habari kila kona ya dunia kuna gonjwa lingine la mfumo wa hewa ambalo ni chagamoto kwa dunia

Sauti
2'25"

24 Machi 2020

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)      

ASSUMPTA:Ni jumanne  ya  Machi Ishirini na nne mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI 

Sauti
12'51"
Madaktari wakifurahi baada ya mgonjwa kupona kutoka hali mahututi kufuatia maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Department of Critical Care Medicine, Affiliated Hospital of Guangdong Medical University

Ondoeni vikwazo kusaidia COVID-19, madaktari wasemao ukweli msiwaadhibu- Bachelet

Wakati idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 ulimwenguni ikizidi kupaa na kuwa zaidi ya 330,000 huku vifo vikifikia 14,652 Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Michelle Bachelet ametaka vikwazo vya kisekta duniani viondolewe ili mataifa yaweza kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo.

Sauti
2'7"