Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika vita dhidi ya virusi vya corona, COVID-19, kitu kikubwa tunaambiwa tuzingatie usafi: Wananchi Geita

Katika vita dhidi ya virusi vya corona, COVID-19, kitu kikubwa tunaambiwa tuzingatie usafi: Wananchi Geita

Pakua

Serikali kote duniani zimeendelea kuja na mbinu za kila namna ili kupambana na janga la virusi vya corona, COVID-19. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa nalo kwa kila namna limeendelea kuziunga mkono jitihada za nchi kote duniani ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo ya namna nzuri ya kupambana na ugonjwa huu, msingi mkubwa ukiwa kwanza utoaji elimu kwa wananchi ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi zaidi. Baraka Fulgence wa Redio washirika Storm FM ya mkoani Geita Tanzania amepita katika mitaa ya mji huo ili kusikia kuhusu uelewa wa wananchi na namna wanavyoipokea elimu ya kupambana na virusi vya corona.

 

Audio Credit
Loise Wairimu/Baraka Fulgence
Audio Duration
3'53"
Photo Credit
©UNICEF/Leonardo Fernandez