Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

7 Septemba 2018

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Siraj Kalyango anaangazia 

Watoto katika vita vya silaha Sudan Kusini na ziara ya Virginia Gamba

Pilika za kuelekea uchaguzi mkuu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na ukiukwaji wa haki za binadamu

Ulinzi wa amani na changamoto zake kwa walinda amani wa Tanzania utamsikia Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga

Makala leo inamulika ujumbe wa amani kupitia muziki

Na katika Kiswahili "usiogope kuuliza kwani kuuliza si ujinga" ungana na mchambuzi Ken Walibora

Sauti
11'38"
UNIC Dar es salaam/Stella Vuzo

Wazungumzao Kiswahili ni zaidi ya milioni 200

Lugha za asili barani Afrika zinaangaziwa tarehe 25 mwezi huu wa Mei, ambayo ni siku ya Afrika.

Kuelekea siku hiyo, kumekuwepo na taarifa ya kwamba lugha ya kiswahili ni ya kwanza kwa kuzungumzwa na watu wengi zaidi ikifuatiwa na Hausa halafu Yoruba.

Jambo lililoibua hoja na mjadala mzito kwenye mtandao wa Twitter, si kuongoza kwa lugha hiyo bali ni idadi iliyowekwa ambayo ni milioni 98.

Ili kusaka ukweli wa hoja hiyo nimezungumza na Profesa Aldin Mutembei, kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumuuliza je takwimu ni sahihi?

Sauti
2'3"
UN News Kiswahili

Joka la mdimu hulinda watundao

Ijumaa ya leo mchambuzi wetu wa neno la wiki ni Ken Walibora ambaye ni mwana riwaya na mwanachama wa Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Anachambua methalo isemayo "joka la mdimu hulinda watundao." Je wewe ni joka la mdimu? Walibora anasema kuwa joka la mdimu ni wale walindao vitu ambavyo mwisho wa siku wala hawawezi kuvitumia. Kwa ufafanuzi wa kina ungana naye.

Sauti
1'3"
UN News Kiswahili

Neno na Wiki- HABA na Onni Sigalla

Katika neno la wiki hii leo, mchambuzi wetu Onni Sigalla ambaye ni Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anachambua neno HABA. Anasema neno hilo mara nyingi huchanganywa na SI na kusomeka kuwa neno moja SIHABA. Hivyo anasema katu si hivyo. Si haba. Anaenda mbali akifafanua visawe vya neno hilo

Sauti
49"

Dawa bandia zaendelea kuleta machungu kwa nchi zinazoendelea

Takribani aina moja ya dawa kati ya 10 zinazotumika katika nchi za kipato cha chini na kati ni bandia au hazijakidhi viwango.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya uliotolewa leo na shirika la afya ulimwenguni, WHO.

WHO inasema taarifa hizo zinamaanisha kwamba watu wanatumia dawa ambazo zinashindwa kutibu au kuzuia magonjwa na hiyo haisababishi tu hasara ya kiuchumi bali pia vifo.

Picha/Worldreader

Kiswahili chetu ndio hazina yetu

Lugha yako ndio mkombozi wako!  Ikiwa leo ni siku ya Afrika, lugha za asili za Afrika nazo zimepigiwa chepuo na miongoni mwao ni lugha ya Kiswahili ambayo barani Afrika pekee inaongoza kwa kuzungumzwa na watu wengi zaidi, idadi ikitajwa kuwa ni zaidi ya watu milioni 200.

Sauti
2'3"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki: UPAKO

Katika neno la wiki hii leo mchambuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA anafafanua neno “Upako”,  Ungana naye...

Sauti
56"