Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

UN News Kiswahili

Neno la Wiki: Mkumbizi

Katika Neno la Wiki hii leo tunaangazia neno “Mkumbizi” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. 

Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana zaidi ya moja, kwanza mtu anayesafisha mahali na kuondoa takataka, watu wengi wanamuita mfanyakazi lakini neno sahihi ni Mkumbizi.  Pili ni mtu afuataye wavunaji shambani na kuokota mavuno yaliyosalia kwa bahati na kutumia kama chakula chake.

Sauti
48"

Neno la Wiki- Mhanga, Manusura na Muathirika

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Mhanga”, "Manusura" na “Muathirika”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo..

Sauti
58"

Neno la wiki: Mhanga, Manusura na Muathirika

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Mhanga", “Manusura” na "Muathirika".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo..

Uwazi utasaidia kuondoa shuku juu ya silaha za maangamizi- Guterres

Tishio la matumizi ya silaha za maangamizi linaongezeka kila uchao licha ya juhudi za kimataifa za kudhibiti na hatimaye kutokomeza matumizi ya silaha hizo.

Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia kikao cha ngazi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichofanyika leo New York, Marekani kuangazia mbinu za kujengeana imani ili kuondoa silaha hizo.

Guterres amesema dunia hivi sasa ina wasiwasi kuwa penginepo silaha za nyuklia zinaweza kutumiwa, hofu ambayo iko kiwango cha juu zaidi tangu kumalizika kwa vita baridi.

Alihesabiwa siku za kuishi lakini akaishi zaidi

Umoja wa Mataifa unaendelea kupigia chepuo usambazaji wa huduma za kujikinga na virusi vya ukimwi, VVU ikiwa ni moja ya utekelezaji wa lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Lengo hilo la ustawi wa afya kwa wote linaangazia siyo tu Malaria na Kifua Kikuu bali pia Ukimwi ambao unaendelea kuwa tishio, licha ya kwamba tayari kuna kinga. Huko nchini Kenya, mwanamke mmoja ambaye baada ya kukatiwa tiketi ya kifo, alikata tamaa akaona dunia imemgeuka. Lakini baada ya kuamua kuchukua hatua, nuru ikaingia na hata akaweza kuongeza familia yake. Je alifanya nini ?