Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walimu wa Kiswahili wamekiri kitabu changu kiliwashawishi kuthamini lugha hiyo adhimu- Walibora

Walimu wa Kiswahili wamekiri kitabu changu kiliwashawishi kuthamini lugha hiyo adhimu- Walibora

Pakua

Shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO limekuwa katika mstari wa mbele katika kuchagiza kuwepo kwa dunia yenye watu wanaojua kusoma na kuandika. UNESCO kwa mtazamo wake unachukulia kupata stadi na kuimarisha stadi hizo za kusoma na kuandika katika maisha kama sehemu muhimu ya haki ya elimu. Matokeo yake yakiwa ni kuwawezesha watu kushiriki kikamilifu katika jamii na kuchangia katika kumarisha maisha yao.

Ili kufanikisha uwezo wa watu kusoma na kuandika vitabu vinakuwa ni muhimu kwani vinajengea uwezo msomaji kuifahamu lugha. Kwa mantiki hiyo waandishi wa vitabu wana nafasi kubwa katika kuathiri uelewa wa msomaji kuhusu lugha lakini pia kusababisha msomaji kupenda au kuikubali lugha hiyo. Matokeo hayo amekiri mwanariwaya kutoka Kenya, Ken Walibora ambaye kazi zake zinatumika kama vitabu vya kiada katika somo la kiswahili nchini Kenya. Grace Kaneiya amezungumza naye na katika awamu ya kwanza ya makala hii hapa anaanza kwa kuelezea safari yake ya uandishi

 

Soundcloud
Audio Credit
Assumpta Massoi/ Grace Kaneiya/ Ken Walibora
Sauti
4'6"
Photo Credit
UNHCR/Catherine Wachiaya