Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya Kiswahili itapanua wigo wa kazi za UN Environment:Msuya

Naibu mkurugenzi mtendaji wa UN Environment Joyce Msuya
UN Environment
Naibu mkurugenzi mtendaji wa UN Environment Joyce Msuya

Lugha ya Kiswahili itapanua wigo wa kazi za UN Environment:Msuya

Utamaduni na Elimu

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UN Environment leo 12 septemba 2019 limezindua tovuti mpya na mitandao ya kijamii kwa lugha ya Kiswahili.

Akizungumzia hatua hiyo naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Joyce Msuya amesema lengo ni kuwafikia mamilioni ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kote duniani , kwani tofuti hiyo ya Kiswahili na mitandao ya kijamii vitatoa taarifa za mazingira, takwimu muhimu na kuelezea hadithi zintakazochagiza za watu wanaofanya kazi kuboresha mazingira ya dunia.

Tovuti hiyo pia itatanabaisha kuhusu mada muhimu zihusuzo matatizo ya mabadiliko ya tabianchi, bayoanuai, suluhu za kiasili, uchaguzi wa hali ya hewa na mengine mengi.

Uzinduzi wa tovuti hiyo mpya ya Kiswahili na mitandao ya kijamii umefanyika siku chache kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi ambao utafanyika jijini New York tarehe 23 Septemba mwaka huu.

Lugha zinaunganisha ulimwengu-UNESCO
UNESCO
Lugha zinaunganisha ulimwengu-UNESCO

 

Shirika la UN Environment ni sauti inayoongoza duniani kuhusu masuala ya mazingira. Linatoa muongozo na kuchagiza wadau kulinda mazingira, kuhabarisha na kuyawezesha mataifa na watu kuboresha hadhi ya Maisha yao bila kuweka rehani mustakbali wa dunia na vizazi vijavyo kimazingira.

Katika kufanikisha azma hiyo UN Environment inafanyakazi kwa karibu na wadau wote zikiwemo serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa  na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kote duniani.