Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© IOM 2021/Lauriane Wolfe

Bia aliyonyweshwa msichana mwingine yageuka mahari ya mtoto na kisha akabakwa!!!

Siku ya kimataifa ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa kibinadamu huadhimishwa kila tarehe 30 ya mwezi Julai. Mwaka huu ujumbe ni Manusura wa  usafirishaji haramu binadamu wawe msingi wa kampeni dhidi ya vitendo hivyo. Hii ni kwa kuzingatia kuwa mara nyingi manusura hupuuzwa,  watu wanashindwa kuwaelewa na hata kile walichopitia huwa hakipatiwi kipaumbele kama njia ya kujifunza, kurekebisha na kuokoa wengine walionasa kwenye mtego huo.

Sauti
3'7"
UN/ John Kibego

Covid-19 imeathiri kazi yangu ya ualimu na sasa ninauza juisi – Mwalimu Catherine Tuhaise 

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kutangazwa na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO, tayari umeweka wazi kuwa kumekuwa na upotevu mkubwa wa ajira duniani. Na utafiti unaenda mbali zaidi kwamba wanawake wataathirika zaidi katika siku zijazo. Hali halisi tayari inaonekana katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu ambako hatua kadhaa zilizochukuliwa ili kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, zimesababisha watu kupoteza vyanzo vyao vya mapato.

Sauti
3'44"
UN/ Jason Nyakundi

Kilio cha sodo au taulo za kike kwa wasichana Nairobi, Kenya chapatiwa jibu

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani, UNFPA linapatia msisitizo suala la wanawake na wasichana kupata taulo za kike au sodo, kwa kuzingatia kuwa ni suala la haki za binadamu. Ukosefu wa vifaa hivyo siyo tu vinashusha utu na hadhi ya mtu pale anapojikuta amechafua nguo zake mbele za hadhira, bali pia humkosesha haki ya kuwa huru kwenda kazini, shuleni. Katika maeneo ya mitaa ya mabanda jijini Nairobi nchini Kenya, wanawake na wasichana wanaoshi katika lindi la umaskini, sodo au taulo za kike ni changamoto kubwa.

Sauti
3'45"
FAO

Vijana na mifumo ya chakula

Katika mada kwa kina hii leo tunamulika vijana na mfumo endelevu wa chakula kwa kutambua kuwa tarehe 26 hadi 28 mwezi huu wa Julai, 2021  huko Roma Italia kutafanyika mkutano wa viongozi kuhusu chakula mifumo ya chakula. Kuelekea mkutano huo wa kuangazia namna ya kuboresha mifumo kuanzia shambani hadi mezani, shirika la Umoja wa Maaifa la chakula na kilimo FAO linaendesha mijadala na wadau mbalimbali wakiwemo vijana.

Nchini Tanzania Devotha Songorwa wa Radio washirika Kids Time FM ameshiriki katika mjadala wa vijana na kuandaa mada hii. 

Sauti
6'36"
UN/ John Kibego

Waganda wahaha kukabiliana na athari za mafuriko na COVID-19

Majanga asili yametishia juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu au SDGs katika nchi zote duniani. Uganda ni miongoni mwa nchi ambazo mwaka huu na mwaka jana 2020 zimeathiriwa moja kwa moja na mlipuko wa COVID-19 na kuongeza chumvi kwenye kidonda cha mafuriko makubwa kihistoria. 

Licha ya changamoto hizo, serikali inawatia moyo wananchi kufanya kazi kwa bidii na kwa busara ili kudhibiti madhara ya majanga haya hasa jamii za ziwani zinazikabiliwa zaidi na majanga hayo mawili wakati mmoja. Makala iliyoandaliwa na John Kibego ina maelezo zaidi.

Sauti
3'43"
UN Kenya/Neil Thomas

Ninatumia nishati ya jua katika ufugaji wa samaki - George Muga

Moja ya masuala yaliyojadiliwa kandoni mwa Mkutano wa ngazi ya juu ya siasa kuhusu maendeleo endelevu unaoendelea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, ni pamoja na namna waafrika wengi wanavyopambana na njia za zamani za nishati na hivyo kutafuta njia mbadala kama vile matumizi ya nishati ya jua. 

Sauti
3'21"
UN/ Jason Nyakundi

Wasichana endelea kufanya kile mnachofanya bila kujali jinsia – Dorothy Kiprop

“Ujasiri wangu wa kuendeleza kipaji changu umewahamasisha wasichana wengine chipukizi kuingia katika sanaa hii ya upakaji rangi na uchoraji”, ni kauli ya Dorothy Kiprop raia wa Kenya muhitimu wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 24. Msichana huyu kupitia mahojiano yaliyofanywa na Mwadishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi, anatoa maoni anatoa ushauri kwa wasichana chipukizi ili waweze kuondoa pengo la usawa wa kijinsia katika kazi zinazoonekana kuwa za kiume katika jamii.

Sauti
2'36"
UN SDGs

Bado usawa wa kijinsia unapaswa kupiganiwa, pamoja na hatua zilizopigwa - Mwandishi wa habari chipukizi

Mwandishi wa habari chipukizi nchini Tanzania, Hadija Halifa ambaye yuko chini ya uangalizi na mafunzo ya Idhaa ya Kiswahili DW ya Ujerumani, akihojiwa na Moses Mghase wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, ameeleza kuwa anatambua kuwa kuna hatua ambazo zimepigwa katika kupunguza pengo lililopo katika usawa wa kijinsia, lakini anapenda kuona mkazo zaidi katika kuondoa kabisa pengo hilo. Kwa mtoto Hadija, anashauri mkazo uanzie katika elimu hususani kwa wasichana.

Sauti
3'14"