Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Covid-19 imeathiri kazi yangu ya ualimu na sasa ninauza juisi – Mwalimu Catherine Tuhaise 

Covid-19 imeathiri kazi yangu ya ualimu na sasa ninauza juisi – Mwalimu Catherine Tuhaise 

Pakua

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kutangazwa na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO, tayari umeweka wazi kuwa kumekuwa na upotevu mkubwa wa ajira duniani. Na utafiti unaenda mbali zaidi kwamba wanawake wataathirika zaidi katika siku zijazo. Hali halisi tayari inaonekana katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu ambako hatua kadhaa zilizochukuliwa ili kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, zimesababisha watu kupoteza vyanzo vyao vya mapato. Mathalani Catherine Tuhaise wa jijini Hoima nchini Uganda ni miongoni mwa walioathirika kwani kufungwa kwa shule nchini humo, kumemkosesha kipato kinachotokana na kazi yake ya ualimu. Mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego amezungumza na Mwalimu huyo ambaye sasa amehamia katika biashara ya kuuza juisi.   

Audio Credit
ANOLD KAYANDA/JOHN KIBEGO
Audio Duration
3'44"
Photo Credit
UN/ John Kibego