Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa hata nikikosa mboga, mimi na familia yangu tunakula mayai - Mnufaika wa mradi wa Lishe Endelevu 

Sasa hata nikikosa mboga, mimi na familia yangu tunakula mayai - Mnufaika wa mradi wa Lishe Endelevu 

Pakua

Pamoja na muongo wa mwisho wa kuelekea katika mwaka 2030 wa kutimiza agenda ya Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs  kuzoroteshwa na vikwazo vya kudhibiti ugonjwa wa COvid-19, mashirika, serikali na watu binafsi kote duniani kwa namna mbalimbali hawajakata tamaa. 

Mathalani nchini Tanzania, kuna mradi wa Lishe Endelevu unaotekelezwa na Shirika la Save the Children kwa ufadhili wa USAID katika mikoa minne Tanzania ambayo ni Dodoma, Iringa, Rukwa na Morogoro kwa lengo la kupunguza Udumavu na kuboresha afya kwa mama na mtoto na hiyo ikiwa inafanikisha lengo namba 2 la SDGs ambalo pamoja na mambo mengine linalenga kuboresha lishe. 

John Kabambala wa redio washirika KidsTime FM ya Morogoro Tanzania amemtembelea mmoja wa wanufaika wa  mradi huo katika Manispaa ya Morogoro ambaye anafuga kuku baada ya kuwa amepatiwa vifaranga 200 vya kuku miezi 6 iliyopita na sasa ameanza kuboresha afya yake, familia na kuinufaisha jamii kiafya na kiuchumi. 

Audio Credit
Anold Kayanda/ John Kabambala
Audio Duration
3'54"
Photo Credit
© World Bank/Arne Hoel