Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bia aliyonyweshwa msichana mwingine yageuka mahari ya mtoto na kisha akabakwa!!!

Bia aliyonyweshwa msichana mwingine yageuka mahari ya mtoto na kisha akabakwa!!!

Pakua

Siku ya kimataifa ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa kibinadamu huadhimishwa kila tarehe 30 ya mwezi Julai. Mwaka huu ujumbe ni Manusura wa  usafirishaji haramu binadamu wawe msingi wa kampeni dhidi ya vitendo hivyo. Hii ni kwa kuzingatia kuwa mara nyingi manusura hupuuzwa,  watu wanashindwa kuwaelewa na hata kile walichopitia huwa hakipatiwi kipaumbele kama njia ya kujifunza, kurekebisha na kuokoa wengine walionasa kwenye mtego huo.

Ni katika muktadha huo, Assumpta Massoi kwa msaada wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM nchini Burundi ameandaa makala hii ambayo ni simulizi ya mtoto mmoja wa kike nchini humu ambaye wakati ana umri wa miaka 12 aliuzwa kwa gharama ya bia na kutumikishwa kingono katika nchi jirani ya Tanzania.  

Audio Credit
Leah Mushi/ Assumpta Massoi
Audio Duration
3'7"
Photo Credit
© IOM 2021/Lauriane Wolfe