Vijana wasichana na wavulana mkoani Mara wasimama kidete kukabiliana na FGM
Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la usawa wa kijinsia, ukipaza sauti hatua zichukuliwe ili kutokomeza kitendo cha ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake, mkoani Mara nchini Tanzania tayari hatua zinachukuliwa na zinazaa matunda. Mafunzo kwenye kituo cha ushirika wa kutokomeza ukeketaji, ATFGM kilichopo kijiji cha Masanga yamekuwa ni chachu ya kutekeleza wito huo kwa kuwa wasichana kwa wavulana wanapata mafunzo ya kuwawezesha kuepukana na tohara na ukeketaji ambao unahatarisha maisha yao.