Ubunifu wa ajira wazaa matunda kwa vijana nchini Burundi
Pakua
Kubuni ajira ni swala linalotatiza pakubwa vijana wengi barani Afrika. Wengi hulalamikia ukosefu wa mitaji au chanzo cha kuanzisha biashara. Lakini wataalamu wa biashara na wachanganuzi wa miradi wanaamini kuwa mtaji mkubwa na wa kuaminika kwanza ni fikra ya biashara pamoja na kujumuika katika shirika.
Kundi moja la vijana wapatao 50 nchini Burundi kwa jina la CVC, baada ya kupokea mafunzo ya mtaalamu wameanza kuona mafaanikio ya biashara yao ilioanza tu na unga wa uji.
Mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani Kibuga ametuandalia makala ifuatayo.
Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/Ramadhani Kibuga
Audio Duration
3'52"