Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake huko Mtwara nchini Tanzania wachukua hatua kujinasua kutoka kwenye umaskini

Wanawake huko Mtwara nchini Tanzania wachukua hatua kujinasua kutoka kwenye umaskini

Pakua

Lengo namba 10 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linaangazia jinsi ya kuondoa pengo la kipato kati ya walio nacho na wasio nacho. Hii ni kwa kuzingatia kuwa ukosefu wa usawa kwenye kipato unaongezeka ambapo asilimia 10 ya matajiri duniani wanamiliki asilimia 40 ya pato la dunia nzima.

Kama hiyo haitoshi, asilimia 10 ya maskini wanapata asilimia kati ya 2 hadi 7 ya pato la dunia nzima. Hali ni mbaya zaidi kwenye nchi zinazoendeleo ambako pengo la ukosefu wa usawa kwenye kipato ni asilimia 11. Umoja wa Mataifa pamoja kupendekeza sera sahihi za kuondoa pengo hilo, unataka ushirikishaji na uwezeshaji wa jamii kwenye shughuli za kiuchumi bila kujali tofauti za kijinsia, kabila na rangi. Na hilo tayari linafanyika huko wilaya ya Masasi mkoani Mtwara nchini Tanzania ambako Edwin Mpokasye wa radio washirika Radio Fadhila FM amezungumza na mjasiriamali mmoja kufahamu kwa kina harakati zake za kujinasua kutoka kwenye umaskini na usaidizi ambao amepata.

 

Soundcloud

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Edwin Mpokasye
Audio Duration
3'41"
Photo Credit
UN News Kiswahili