Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wasichana na wavulana mkoani Mara wasimama kidete kukabiliana na FGM

Vijana wasichana na wavulana mkoani Mara wasimama kidete kukabiliana na FGM

Pakua

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la usawa wa kijinsia, ukipaza sauti hatua zichukuliwe ili kutokomeza kitendo cha ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake, mkoani Mara nchini Tanzania tayari hatua zinachukuliwa na zinazaa matunda. Mafunzo kwenye kituo cha ushirika wa kutokomeza ukeketaji, ATFGM kilichopo  kijiji cha Masanga yamekuwa ni chachu ya kutekeleza wito huo kwa kuwa wasichana kwa wavulana wanapata mafunzo ya kuwawezesha kuepukana na tohara na ukeketaji ambao unahatarisha maisha yao. Elimu hiyo imewaingia vyema kiasi kwamba wavulana nao wanasaidia kuepusha wasichana wasikeketwe kama makala hii iliyowezeshwa na Warren Bright wa shirika la Idadi ya watu duniani,  UNFPA nchini Tanzania inavyoweka bayana. Msimulizi ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
Grace Kaneiya/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
Warren Bright/UNFPA Tanzania