Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwalimu wa kike aanzisha biashara inayotoa fursa za ajira kwa wengine Uganda

Mwalimu wa kike aanzisha biashara inayotoa fursa za ajira kwa wengine Uganda

Pakua

Wanawake wanajumuisha takriban asilimia 52.5 ya nguvu kazi na ni kiungo muhimu katika kufanikisha melengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan katika sekta ya ujasiriamali kwenye biashara ndogo ndogo na za wastani. Hata hivyo, wanawake kwa kawaida hukabiliwa na changamoto nyingi ikilinganishwa na wanaume katika kuanzisha, kusimamia na kukuza biashahra hizo kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kazi ulimwenguni, ILO, iliyoangazia uwekezaji wa wanawake na mapendekezo nchini Uganda mwaka 2014. Mazingira duni husababisha wanawake wajikute njiapanda kwa sababu za kiutamaduni, vikwazo kisheria, na mtazamo wa wanawake kuhusu wajibu wao hususan nyumbani. Licha ya vikwazo hivyo lakini jamii imepata mwamko na wanawake wanahamasishwa na wenyewe wanahamasika kuanzisha biashara kwa mfano katika makala hii iliyoandaliwa na kuletwa kwako na mwandishi wetu kutoka Hoima nchini humo, John Kibego.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'59"
Photo Credit
UNIC/Stella Vuzo