Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Natumia uelewa wangu kuhusu mauaji ya halaiki kuepusha yasiyotokee tena- Mwanafunzi Tanzania

Natumia uelewa wangu kuhusu mauaji ya halaiki kuepusha yasiyotokee tena- Mwanafunzi Tanzania

Pakua

Miaka 74 tangu kukombolewa kwa kambi ya mateso na mauaji ya wayahudi milioni Sita huko  Auschwitz-Birkenau, nchini Poland yaliyofanywa na manazi wa Ujerumani, bado kuna ubaguzi kwa misingi mbalimbali iwe ya kidini au kikabila. Hali hii  hutia sana wasiwasi Umoja wa Mataifa ambao uliamua siyo tu kutenga siku ya kimataifa ya kumbukizi ya mauaji hayo ya halaiki dhidi ya wayahudi kama fursa ya kukumbuka na kutathmini, bali pia kuwa na programu maalum ya kuelimisha jamii juu ya madhila ya mauaji ya aina hiyo na viashiria vyake ili kuepusha yasitokee tena. Programu hizo zinafanyika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania ambako wakati wa kumbukizi ya mwaka huu ya mauaji ya halaiki dhidi ya wayahudi, wanafunzi walionyesha ubobezi wao juu ya suala hilo na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam amezungumza na Vanessa Innocent Mpinga, mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Chang'ombe jijini humo baada ya wanafunzi kushiriki kumbukizi ya mauaji ya halaiki ambapo Vanessa anaanza kwa kuelezea uelewa wake.

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
4'5"
Photo Credit
UN