Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoto yangu imetimia, nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu- Mtoto Rehema

Ndoto yangu imetimia, nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu- Mtoto Rehema

Pakua

Hatimaye mtoto Rehema Paul ambaye aliponea chupuchupu kuajiriwa kazi za ndani baada ya mwajiri wake kubaini kuwa umri wake  haukuwa unaruhusu kufanya kazi, sasa ameanza masomo katika shule ya msingi Mchikichini, kwenye manispaa ya Morogoro nchini Tanzania. Mwajiri huyo, Herieth Mkaanga amefurahi sana kwani amefanikisha lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la kutaka elimu kwa watoto bila ubaguzi wowote ule na wakati huo huo kufanikisha ndoto ya mtoto Rehema ya kupata elimu. Wiki iliyopita tulikupatia simulizi yenyewe mwanzo wake na leo katika sehemu hii ya pili na   ya mwisho, JOhn Kabambala wa Radio washirika Kidstime FM kutoka TAnzania amefuatili kwa kina safari yao ya kufika shuleni na kuanza masomo. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/John Kabambala
Audio Duration
4'24"
Photo Credit
UN/maktaba