Watu Asili kushiriki na kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai: Burundi
Kongamano la watu asili kutoka eneo la Maziwa makuu barani Afrika limehitimishwa mjini Bujumbura Burundi . Lilijikita katika jinsi Jamii hiyo wanavyoweza kushiriki na kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai katika maeneo wanakoishi.
Jamii hiyo imekuwa inanyooshewa kidole kwa kuhusika na sehemu kubwa katika uharibifu wa mazingira, madai ambayo wanayakana wakitaja kwamba mazingira ni sehemu ya maisha yao.