Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwanda vidogovidogo vyalaumiwa kuchafua vyanzo vya maji

Viwanda vidogovidogo vyalaumiwa kuchafua vyanzo vya maji

Pakua

Maji safi na salama ni uhai wa viumbe vyote ulimwenguni ikijumuisha binadamu, wanyama na mimea. Lengo namba 6 la  malengo ya maendeleo  endelevu, SGD linazungumzia maji safi na salama kwa kila mtu ifikapo  ya mwaka 2030.

Katika migogoro ya kimazingira, viwanda vidogo na vikubwa vimekuwa vikilalamikiwa kuharibu mazingira kwa kujenga mifereji inayopeleka maji taka katika vyanzo vya maji au mito.

Mwandishi wetu John Kibego kutoka Uganda ameshuhudia mgogoro katika wilaya ya Hoima nchini humo ambako wanavijiji wanalalamika kuwa mito yao imeharibiwa na maji taka kutoka katika  kiwanda kimoja cha pombe. Nini kimetokea katika mgogoro huo? Fuatilia mkasa huo….

Audio Duration
3'55"
Photo Credit
Utekaji maji nchini Uganda.Picha:John Kibego